Tottenham ilitoka nyuma na kuishinda
kilabu ya ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza Sheffield United na
kuweka tarehe na Chelsea katika fainali ya kombe la League Cup mnamo
tarehe mosi mwezi Machi.
Hii ni baada ya mchezaji Christian
Eriksen kufunga bao la dakika za mwisho.Mkwaju wa adhabu uliopigwa na
Ericksen uliifanya Totenham kuwa kifua mbele kwa mabao shinda 2-0.
Hatahivyo
mchezaji wa Sheffield mwenye umri wa miaka 18 Che Adam alifunga mabao
mawili akiwa karibu na eneo la hatari katika kipindi cha dakika tatu na
kuweka matumaini ya mda wa ziada kuongezwa.
Lakini Eriksen alipata bao la ushindi na kufanya mambo kuwa 3-2.
Spurs
iliicharaza Chelsea katika fainali ya kombe hilo mwaka 2008 na timu
hizo mbili zitakutana tena katika uwanja wa Wembley,siku tatu kabla ya
Tottenham kukabiliana na Firentina katika michuano ya kuwania kombe la
Yuropa.BBC
Post a Comment