Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Krispin Meela |
Na Mwandishi wetu ,Rungwe
MVUTANO wa
kimaslahi unaoendelea katika Shule ya Sekondari ya watoto yatima ya
Mwaji, juu ya nani muazilishi wa shule hiyo, iliyopo Wilayani Rungwe
Mkoani Mbeya, umechukua sura mpya baada ya serikali ya Wilaya kudaiwa kumpiga
marufuku mmoja wa kiongozi ambaye inasemekana ni muazilishi halali wa shule
hiyo kutokanyaga katika eneo hilo.
Sambamba
na muazilishi huyo kuzuiwa kufika kwenye eneo hilo, pia serikali hiyo
imewaondoa watoto yatima zaidi ya 60 kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mbeya,
kuendelea kupata elimu katika shule kutokana na sababu ambazo hazijawekwabayana
katika uongozi wa shule hiyo.
Hatua hiyo
imetajwa kuwaathiri walezi wa watoto hao,ambao wengi wao wameachwa na
wazazi hivyo kulelewa na ndugu na jamaa ambapo kiuchumi hawako vizuri hivyo
kuitegemea shule hiyo ambayo imekuwa ikipokea misaada kutoka nchini Marekani.
Elifa
Mwakatobe, ni mwanzilishi na mmiliki wa shule ambaye Mkuu wa Wilaya ya
Rungwe, Chrispine Meela , amempiga marufuku kukanyaga shuleni hapo, alisema
yeye ameshangazwa na kauli zinazotolewa na kiongozi ambaye amebeba dhamana ya
kuiongoza Wilaya hiyo kuwa na viashiria vya uchochezi na zinazohamasisha
vurugu badala ya kutatua tatizo lililopo.
Amesema,
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2004 na kupata usajili kutoka Baraza la mitihani
mwaka 2013 ikiwa chini ya uazilishi wake kwa kushirikiana na raia kutoka nchini
Zambia Marehemu Raphael Fili Mwaji hivyo anashangazwa na hatua ya serikali
kumzuia kutofika eneo hilo la shule sambamba na kutoshughulika na jambo lolote
linaloihusi shule hiyo.
Akizungumzia
sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Meela alikiri kuwepo kwa mgogoro
huo na kukanusha madai ya kwamba yeye anamaslahi binafsi ndani ya shule
hiyo isipokuwa anasimamia sheria na taratibu katika Wilaya yake.
Alisema,
sababu ya kumpiga marufuku kufika shuleni hapo, ni kwamba mama huyo
amefungua shule nyingine na kutumia nyaraka za usajili wa shule ya Mwaji
kukusanya ada pamoja na michango mbalimbali kutoka kwa walezi, jambo
linalodhihirisha kwamba ni tapeli.
Hata
hivyo, inadaiwa kuwa Elifa Mwakatobe, aliwahi kuwa Mwenyeikiti wa kikundi cha
Bujela ambacho ndicho kinachomiliki shule hiyo ya Mwaji kwa sasa ambayo ipo
chini ya shirika la MOP na kwamba alijitoa siku nyingi kabla ya shule hiyo
kupata usajili.
Mwisho.
Baadhi ya wanafunzi wanaolelewa na kituo hicho cha Mop |
Elifa Mwakatobe, ni mwanzilishi na mmiliki wa shule ambaye
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispine Meela , amempiga marufuku kukanyaga
shuleni hapo
|
jengo linatumiwa na wanafunzi wa kituo hicho mara baada ya kudaiwa kutimuliwa na uongozi wa shule ya Bujela |
Jason Swila Mkuu wa shule ya Bujelwa ambayo ipo katika mgogoro huo. |
Wwelodi Michael Nzowa mmoja wa viongozi wa kikundi hcho cha Mop. |
Post a Comment