Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Saza Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Ndugu Epani Raphael (10) amekutwa amekufa maji kwenye korongo la  maji alimokuwa anaogelea na wenzake.

Mwili wa marehemu  05.01.2015 majira ya saa 12:00 jioni huko katika kijiji  cha  saza, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya.

Inadaiwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni baada ya mwanafunzi huyo huyo kuzidiwa maji na kushindwa kuogelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed  Msangi anatoa wito kwa wazazi/walezi kuwa makini na watoto wadogo kwa kutoa/kuweka uangalizi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kutowaruhusu kuogelea katika mito, mabwawa kwani ni hatari kwa maisha yao hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali teule ya mwambani wilaya ya chunya kwa uchunguzi wa kitabibu.

Wakati huo Jeshi la Polisi Mkoani mbeya linawashikilia watu wawili wakiwa na silaha bunduki aina ya shot gun yenye namba co 57126 iliyoachanishwa, mtutu ukiwa kwenye bomba la maji  na kitako kimefichwa kwenye begi la nguo.

 Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Ndugu Ahmed Msangi  amewataja watu hao kuwa ni  Isack Mwampashi (26) mkazi wa sae- jijini mbeya na Desdelius Mzogola (42) mkazi wa Ihanga –njombe

Watuhumiwa walikamatwa  04.01.2015 majira ya saa5 usiku huko eneo la Mpakani- check point, kata ya Igawa, tarafa ya rujewa, wilaya ya mbarali, mkoa wa mbeya wakiwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili T.173 cyj aina ya king lion wakitokea mbeya kuelekea njombe vijijini.

Imeelezwa kuwa watu hao walikuwa wakielekea  nyumbani kwa Mmelu Mmgala Mkazi wa Njombe vijijini ambapo taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

Mwisho.   

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top