Kocha Mkuu Tanzania Prisons David Mwamwaja |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Licha ya klabu ya Tanzania Prison kuendelea kuchechemea katika
ligi kuu Vodacom Tanzania bara kwa kupata matokeo mabaya kocha wa timu hiyo
Ndugu David Mwamaja ameibuka na kudai kuwa timu yake ni bora nakwamba itafanya
vyema katika mechi zinazofuata.
Mwamaja, ambaye ameweza kujitengenezea jina
baada ya kuinusuru timu hiyo kushuka daraja katika msimu uliopita, ameiambia blog
hii kuw hawezi kukata tamaa kwa matokeo hayo aliyoyapata baada ya kucheza mechi
mbili zaidi yamempa chachu ya kujipanga upya.
Amesema pamoja na kwamba timu
yake imeshika nafasi ya mwisho katika msimso wa ligi lakini bado kuna matumaini
makubwa ya kutoka katika nafasi hiyo kutokana na timu zote kuto achana kwa
mbali katika pointi.
Amesema katika mchezo wake na
Ndanda Fc ya Mtwara amegundua mapungufu madogomadogo ambayo hata hivyo
amekwisha yafanyia kazi mara baada ya kukutana na wechezaji wake.
Amesema, sababu kubwa
iliyochangia kwa kikosi hicho kufanya vibaya dhidi ya Ndanda Fc, yalitokana na
kukosekana kwa mchezaji kiungo mshambuliaji Fred Chudu ambaye alikuwa
akitumikia adhabu baada ya kupata kadi tatu za njano.
Amesema, kutokana na kasoro
hizo, amejipanga vizuri na kwamba tayari amekutana na wachezaji na kuzungumza
nao na kuwaeleza nini wanachotakiwa kufanya na kusahau maumivu waliyoyapata
zaidi wasonge mbele.
Aidha, wakati kocha huyo
akielezea hayo, blog hii imemepata
taarifa za ndani kutoka kwenye uongozi wa Timu hiyo, kwamba huenda kocha huyo
asipate nafasi tena ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa
kikao hicho pia kilipata nafasi ya kupendekeza majina ya makocha watatu,
miongoni mwao wakiwemo kocha Saleh Bausi ambaye ni kocha msaidizi wa Mbeya
City, Selemani Matola ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Simba.
Akizungumzia, tetesi za
kuondolewa kwa kocha huyo, Katibu wa Prisons, Oswald Moris,alisema ni kweli
uongozi ulikutana lakini mambo yaliyojadiliwa ndani ya kikao hicho ni
kuangalia,jinsi timu itakavyojiondoa kwenye adha hiyo na wala kikao hicho hakijamzungumzia
kocha.JAMIIMOJABLOG
Mwisho.
Post a Comment