Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.

Na Mwandishi wetu ,Dar es salaam
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe,amewaonya
 wapinzani nchini kwa kusema kuwa wasijidanganye kuwa matukio
 ya vurugu wanayoyafanya kwenye chaguzi mbalimbali
 hayatasaidia kuking’oa  Chama Cha Maopinduzi (CCM)
 madarakani kwasababu Tanzania siyo sawa na Somaria.

Akizungumza katika mahojiano na redio moja hapa nchini
 kufuatia taarifa zilizoripotiwa na gazeti moja  kwamba  alitaka kupigwa  wakati wa
 uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Kyela.

Dk.Mwakyembe alisema kinachofanywa na wapinzani ni utoto wa
 kisiasa ambao wanadhani kuwa kufanya fujo ndiko
 kutaviwezesha vyama vya upinzani kushika hatamu ya uongozi.
 -“ Kinachiofanywa na wapinzani ni utoto wa kisiasa 
 huwezi kupata uongozi kwa kufanya fujo, Tanzania siyo
 Somaria, wanajidanganya na pia wanajimaliza sababu
 Watanzania hajazowea mambo ya vita,”alisema.

Alisema kilichotokea juzi wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti
 wa Mamlaka ya Mji wa Kyela ni uelewa mdogo wa sheria kudhani
 kuwa mbunge hawezi kushiriki kupiga kura katika mkutano wa
 Baraza la Mamlaka ya Mji.

Dk Mwakyembe alisema viongozi, wanachama na na wafuasi wa
 vyama vya upinzani wasome sheria badala ya kujenga hoja
 hafifu ambazio hazina mashiko na kufanya vurugu kwa kudhani
 kuwa  kufanya huivyo kutawarahisishia kupata madakaka
 .
 Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji wa
 Kyela, Raphael Samweli ‘, alisema uchaguzi wa mwenyekiti
 wa mamlaka hiyo uliahirishwa kutokana na wajumbe wa Chadema
 kushindwa kuelewa sheria ya mamlaka ya miji inaeleza nini
 kuhusu wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya Mji.

Samweli alisema kwa mujibu wa sheria ya namba 45 ya mamlaka
 ya mji inaeleza kuwa wajumbe wa baraza la Mamlaka ya Mji ni
 pamoja na mbunge wa jimbo husika,madiwani watatu wa
 kuteuliwa, wenyeviti wa vitongoji,na  wenyeviti wa
 vitongoji wa kuteuliwa.

Alisema viongozi wote hao  sheria inawaruhusu kupiga
 kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji na makamu
 hivyo haoni sababu ya Chadema kugomea sheria hiyo ambayo ipo
 wazi.
 Samweli alisema kutokana na wajumbe wa Chadema kutofahamu
 sheria hiyo waliomba zoezi la kuchagua mwenyekiti wa 
 Mamlaka ya Mji wa Kyela liahjrishwe  hadi wapate
 tafsili ya sheria kutoka kwa wanasheria wao.

Hata hivyo, taarifa zilizopo ni kwamba hatua ya Chadema
 kugomea uchaguzi huo inatokana na taarifa waliyokuwa
 wamewaeleza wananchi wa Kyela kupitia mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Mbeya Mjini. Joseph Mbilinyi
 maarufu Sugu na kueleza kuwa mamlaka ya mji wa Kyela itakuwa
 chini ya Chadema .

Kutokana na hali hiyo viongozi wa Chadema wanahofu
 watawaeleza nini wananchi kama uchaguzi ukifanyika halafu
 mamlaka hiyo ikashindwa kuwa chini ya Chadema.
 Mwisho.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top