JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Ofisi ya Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,
Fax - +255252503734 MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 02.11.2016.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu, ajali za barabarani na kumakata mali mbalimbali.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 14.10.2016 hadi tarehe 30.10.2016 lilifanya misako mbalimbali katika maeneo ya Jiji la Mbeya. Misako hiyo ilifanyika maeneo ya Airport, Block T, Iyela, Mwanjela, Ilomba, Uyole na Mwakibete. Katika Misako hiyo iliyolenga kukomesha vitendo vya wizi na uvunjaji wa nyumba nyakati za usiku na mchana pia unyang’anyi wa kutumia nguvu na silaha. Aidha misako hiyo ilifanyika mikoa ya Songwe na Iringa kwa lengo la kukamata watuhumiwa wengine.
Mafanikio yaliyopatikana katika misako:
Kupatikana kwa Mali za Wizi: Katika misako hiyo, mali na vitu mbalimbali vya wizi vilipatikana ambavyo ni:-
Flat Screen 23 za aina mbalimbali kama ifuatavyo:-
Samsung inch 55 curve moja
Samsung inch 32 nne
JVC inch 55 moja
BOSS inch 42 moja
Samsung inch 48 mbili
Sony inch 48 moja
LG inch 32 mbili
Rising inch 42 moja
TCL inch 32 mbili
Singsung inch 32 moja
Singsung inch 25 moja
Samsung inch 27 moja
Kodtech inch 25 moja
Pintech inch 32 moja
Mr. UK inch 25 moja
King hong solar inch 25 moja
JVC inch 48 moja
Home Theater za aina mbalimbali
Panasonic moja
LG moja
Sony nane
Sea Piano mbili
Rising moja
Pintech moja
Technosonic moja
Samsung mbili
Zote zikiwa zimekamilika.
Laptop tano aina ya
Dell tatu
Toshiba moja
HP moja
Kompyuta [Desk Top] mbili aina ya Dell
Deck za Video nne
Singsung mbili
Ailing moja
Panasonic moja
Saa ya Ukutani moja aina ya Quartz.
Majiko ya Gesi madogo 03 aina ya ORYX
Meza ndogo 03
Radio za kawaida mbili aina ya Panasonic na Sony.
King’amuzi 01
Stablizer 01
Pasi za Umeme 02
Thermos 02
Blanket kubwa 03
Remote Control 10 za aina mbalimbali
Vibegi vidogo 06
Mabegi makubwa 03
Aidha upelelezi wa majalada ya kesi hizi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa.
Kukamatwa Watuhumiwa 15 wa Uhalifu: Aidha katika misako hiyo watuhumiwa 15 walikamatwa na kukiri kuhusika katika matukio ya wizi, uvunjaji wa nyumba usiku na mchana na kuiba ambapo majalada ya uchunguzi yalifunguliwa. Majalada 08 ya kuvunja nyumba usiku na mchana na kuiba yalifunguliwa na majalada 02 ya unyang’anyi wa kutumia silaha yalifunguliwa. Watuhumiwa hao ni pamoja na:-
1. FRIDAY MBWIGA (20) Mkazi wa Airport
2. ZAKARIA JACKSON (24) Mkazi wa Airport
3. SAID GEORGE (24) Mkazi wa Airport Nkwenzulu
4. BARAKA KIBONA (26) Mkazi wa Simike
5. SALUM ATHUMAN (23) Mkazi wa Vwawa Viwandani
6. GOODLUCK CHAULA (20) Mkazi wa Airport
7. ALEX SIKALENGO (23) Mkazi wa Airport
8. DISMAS ASAJILE (19) Mkazi wa Manga – Mwanjelwa
9. LAZARO GODWIN KITWIKA (20) Mkazi wa Mwanjelwa
10. GODFREY MDOKWA (20) Mkazi wa Airport
Aidha watuhumiwa wengine 05 waliouziwa mali za wizi walikamatwa katika misako hiyo ambao ni:-
BONIFASI MWAIHOJO (27) Mkazi wa Juhudi - Ilemi
IMANI KOMPAUND (24) Mkazi wa Uyole ya Kati
AIZACK MBOYA (26) Mkazi wa Karoleni Tunduma
LAZARO JOHN SIAME (29) Mkazi wa Tazara Tunduma
IBRAHIM SALUM (27) Mkazi wa Mwangota Iringa
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa jamii hasa vijana kuacha tabia ya kutaka kupata mali au utajiri kwa njia ya mkato na badala yake wafanye kazi halali ili wapate kipato halali. Pia anasisitiza kuwa maendeleo hayapatikani kwa kufanya kazi hama biashara haramu, watumie fursa zilizopo Mkoa wa Mbeya kujitafutia ajira. Aidha anatoa wito kwa wakazi wa Mbeya walioibiwa vitu vyao kufika kituo cha Polisi Kati (Central Police Station) kwa ajili ya utambuzi wa mali zao.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment