Mahakama
ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki Judith Wambura
maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media
Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
Hukumu
hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa imefunguliwa na
viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith Wambura
kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.
Awali
mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai Oktoba 13
mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka huu
kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.
Katika
kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba mahakama
itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni
kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru
aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara
ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.
Judith
Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye baadhi ya magazeti
uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa
kabla ya Ruge na Kusaga.”
Wakati
akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee wa upande
wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama imemtaka aombe radhi
kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa nchini na
ikiwezekana duniani pia
Post a Comment