Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Na Emanul Madafa,Mbeya
ASKARI polisi mwenye
cheo cha Sajenti, D 4179 Partick Gondwa (54), amejiua kwa kujipiga risasi akiwa
ndani ya kituo cha polisi na kusababisha kifo chake papo hapo Wilayani Mbozi
Mkoani Mbeya.
Askari huyo ambaye, pia ni mtunza vielelezo kwenye kituo
hicho cha Polisi Wilaya ya Mbozi, inasemekana alijipiga risasi ndani ya kituo
hicho kwa kutumia bastola ambayo nayo pia ni kielezo kilichokuwemo ndani ya
chumba hicho.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,
alisema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa za usiku huko katika kituo cha
polisi cha Mbozi , ambapo inasemekana kwamba marehemu huyo aliingia ndani ya
chumba cha kuhifadhia vielezo, kisha kuchukua bastola na kujipiga kwenye kichwa
chake.
Amesema Maelezo ya awali ni kwamba askari huyo, alifika ndani ya kituo
majira ya saa tisa za usiku na kuingia kwenye moja ya chumba cha vielelezo na
kuchukua bastola na kisha kuielekeza kwenye mdomo wake na kuifyatua.
Msangi, aliendelea kufafanua kwamba, inadaiwa kwamba askari
huyo alipoingia ndani ya chumba hicho alikaa chini na kuuelekeza mdomo wa
bastola kwenye kinywa cha mdomo kisha kuifyatua
hali iliyosababisha kufumua kichwa chake na kusababisha umati wake papo
hapo.
Aidha, Kamanda Msangi, alisema kuwa chanzo cha tukio hilo
kinachungwa na kwamba mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa
ndugu na jamaa tayari kwa maziko.
Marehemu huyo, ameacha mke na watoto na kwamba ni mwenyeji wa Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mwisho.
Post a Comment