Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa ndani jumba bovu baada ya kufanyiwa unyama na watu wasiofahamika.
Na Emanuel Madafa,Mbeya
MTOTO wa miaka nane( 8) mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya jina linahifadhiwa , amepoteza maisha baada ya kubakwa hadi kufa na watu wasiojulikana.

Mwili wake umekutwa kwenye pagale la nyumba (Ghofu) ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea  lililopo ndani ya moja cha chumba kilichopo ndani ya nyumba hiyo ambayo ujenzi wake bado haujakamilika.

Kamada wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wahusika wa tukio hilo wanatafutwa.

Akizungumza na Blog hii kwenye eneo la tukio, Balozi wa Mtaa wa Ilomba uliopo ndani ya Jiji la Mbeya, Azekiel Mwakalundwa, alisema taarifa za mauaji hayo ya kikatili aliipata jana(leo) asubuhi majira ya saa moja kutoka kwa majirani waishio karibu na eneo la nyumba hiyo.


Amesema, baada ya kushuhudia tukio hilo, alitoa taarifa polisi ambao walifika na kuchukua mwili wa mtoto huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kwa upande wake, mama  mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema  mtoto huyo alitoweka nyumbani ,January 7 mwaka huu nakwamba aliaga kuwa anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji iliyopo umbali kidogo na nyumbani.

Amesema, hali ya hofu ilianza kumuingia baada ya kupita masaa kadhaa bila ya mtoto huyo kurejea ndipo alipoamua kumtuma mtoto mwingine kwenda kumuita lakini alirejea na kudai kuwa hajamuona.

Hata hivyo, pembeni  ulipolazwa mwili wa mtoto huyo, kulikutwa ndoo ambayo ndani yake kulikua na nguo za shule alizokuwa amekwenda kuzifua.

mwisho



Majirani wakishuhudia tukio hilo
Askari polisi wakitoa mwili wa marehemu ndani ya jumba hilo kwa ajili ya kwenda kuhifadhia hospital ya rufaa mbeya kwa uchunguzi zaidi





Majirani wa mtaa wa Ilomba eneo la Itemba  Veta jijini Mbeya wakiwa hawaamini kilichotokea katika eneo hilo




Pagala ambalo ndiko unyama huo umefanyika



Mama mlezi wa binti huyo Bi.Sala Mwandopo akilia kwa uchungu









maeneo ambayo ni hatari zaidi katika eneo hilo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top