Katika hali ya kushangaza, polisi walijikuta wakipata shughuli pevu
kumkamata staa asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ambaye alidaiwa
kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha pasipo kuwa na kibali, Amani
linakupa mchapo.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita, nyumbani kwa mwigizaji huyo,
Kijitonyama jijini Dar kulikokuwa na bethidei ya rafiki yake
aliyejulikana kwa jina moja la Neema.
Awali, mapaparazi wa GPL walipokea simu ya mmoja wa majirani wa Wema
ambaye alidai mwigizaji huyo amekuwa na tabia ya kufanya sherehe kwake
na kufungulia muziki mkubwa ambao unasababisha kero.
“Kwa kweli ni kero, kila mara amekuwa na tabia ya kupiga muziki
mkubwa katika sherehe zake ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama jana
(usiku wa Jumatatu) muziki ulifunguliwa kuanzia saa mbili usiku mpaka
asubuhi na majirani walimfuata Wema mara kadhaa kumtaka apunguze sauti
lakini aliwajibu vibaya.
“Njooni mshuhudie wenyewe, tumeita polisi wamkamate,” alisema jirani mmoja.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
Mapaparazi wetu walichukua usafiri wa pikipiki na kuwahi fasta na kukuta polisi wakihangaika kwa muda mrefu kumkamata mrembo huyo lakini ikashindikana kwa kuwa alikuwa amelewa na kukimbia hovyo huku akiwa nusu utupu.
“Kwa sababu hiyo walimkamata mmiliki wa muziki ambaye jina lake
halikupatikana mara moja na mwenye sherehe (Neema) kisha kwenda nao
katika ofisi za mtendaji, Kijitonyama kwa ajili ya hatua za kisheria,”
alisema.
Akizungumza na GPL, mwenyekiti wa mtaa huo, Mzee Haogwa,
alithibitisha kuletewa malalamiko ya Wema na kufika nyumbani hapo ambapo
pia alidai alishangazwa na kitendo cha kuwakuta wanaume tata kwenye
sherehe hiyo.
Picha: Timu iliyofika nyumbani kwa Wema Sepetu kumkamta kwa usumbufu
aliosababisha kwa majirani.Wakachikua spika na kumbeba mwenye sherehe,
Neema( rafiki wa Wema Sepetu) kwenye bajaji.
GPL
Post a Comment