![]() |
| Sehemu wa washiriki wakiw katika Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. |
![]() |
| Mmoja wa wadau wa Mkutano huo akichangia mada. |
![]() |
| Picha ya pamoja. |
Na Chalila Kibuda
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd,amesema watu wegi waonaishi maeneo ya mijini katika Afrika na dunia nzima wanapata changamoto ambazo ni lazima ziainishwe katika kuweza kuzikabili.
Balozi Idd ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kikanda uliowakutanisha viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika Mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika na jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050,uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
‘’Maeneo ya mjini katika Afrika yana fursa lakini maeneo hayo yana changamoto kutokana na ukuaji wa uchumi pamoja na mwingiliano wa kijamii’’amesema Balozi Idd.
Amesema maeneo ya mijini na majiji ni vituo vya fursa za uchumi,Teknolojia na sehemu ya kubadilishana mawazo na uzoefu na kufanya watu wa vijijini kuvutika zaidi wakiwemo vijana kukombilia mjini kwa ajili ya urahisi wa kupatikana kwa fursa pamoja na huduma mbalimbali.
Balozi Idd amesema watu wanaokwenda katika majiji wanajifunza njia mpya za kuishi na kufikiria jinsi ya kuendesha maisha yao kutokana na kuwepo hali hiyo majiji yanapambana dhidi ya umasikini na kuweka mikakati bora ya kuendesha majiji hayo.
Aidha amesema kushindikana na uimara katika miji na majiji matokeo yake ni umasikini unaingia ,magonjwa na kuwepo hali hiyo inaleta maswali ambayo yanatakiwa kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kuyatatua.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu,Profesa Joseph Semboja amesema jukwaa hilo la leo ni kuangalia changamoto na fursa mbalimbali zinazoletwa na ukuaji wa miji ya ukanda wa Afrika Mashariki na jinsi ya viongozi wa Afrika wanavyoweza kukabiliana nazo kwa pamoja.
‘’Kuna changamoto na uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika na duniani kwa ujumla wanaoishi mijini na kusababisha msongamano na shinizo la nyumba ,ajira huduma za kijamii’’amesema Prof.Semboja.

Post a Comment