Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Na Mwandishi wetu,Mbozi
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi, amejikuta katika wakati mgumu, baada ya wananchi wa kata ya Halungu, Wilayani Mbozi, kumzomea wakimtaka kueleza lini watalipwa fedha zao walizoiuzia serikali mahindi.

Tukio hilo lilitokea juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo, baada ya Naibu Waziri huyo, ambaye ni mbunge wa jimbo hilo la Mbozi na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, alipokuwa akijibu maswali ya wananchi katika mkutano wa hadhara.


kabla ya kuanza kwa maswali hayo, Naibu Waziri huyo alipata nafasi ya kutoa hotuba yake ambayo iliibua hisia kwa baadhi ya wananchi ambao walianza minong'ono ya chini kwa chini.


Hata hivyo, baadhi ya wananchi walionekana kukerwa na hotuba hiyo ambayo haikuonesha matumaini ya wakulima hao kulipwa fedha zao baada ya kuikopesha serikali mahindi, hali iliyowalazimu wahusika wa mkutano kutoa nafasi kwa wananchi kuuliza maswali.



Miongoni mwa wananchi waliouliza maswali  ni Lamson Nkota, ambaye alimbana Naibu Waziri huyo kueleza sababu za wakulima kushindwa kulipwa deni baada ya kuiuzia serikali mahindi.

Akijibu swali hilo, Zambi alisema kuhusu suala la kukwama kwa mbolea ya ruzuku , lilitokana na changamoto ya kibajeti, pamoja na kushindwa kwa mfumo ulionzishwa wa kutoa mbolea hiyo kwa vikundi na kwamba serikali imejipanga na msimu ujao mambo yataenda vizuri.

"Lakini kwa hili la mbolea ya Tanzania kuwa ghari wakati nchini Malawi ambapo mbolea yao hupita bandari ya Dar es salaam ni ndogo.....hili ni swali ambalo linatumiwa kimakosa, pengine kwa kupotishwa kwani inawezekana hali hiyo inajitokeza kutokana na kutofautiana kwa mifumo ya kodi" alisema Naibu Waziri Zambi.

Kuhusu suala la malipo ya mahindi, Zambi alisema kuwa tayari serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 15 ambazo zitaanza kulipwa kwa wakulima hivi karibuni.

Alisema fedha hizo ni kati ya shilingi Bilioni 70 zilizokuwa zikidaiwa baada ya wakulima kuuza mahindi yao kwa serikali kupitia kitengo chake cha wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (Nfra).

"Sasa ndugu zangu kama mnasema mimi sijawasaidia na kuja kunihukumu hapa kwa kunizomea, mtakuwa hamnitendei haki ...kwani hata kwa Wilaya ya Mbozi baada ya kutambua kuwa mmezalisha sana mahindi nilishawishi mkapewa mgao wa tani 15 kiasi kikubwa kuliko wakulima wenzenu wa nikoa yote ya Nyanda za juu kusini.

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top