Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kikosi kazi cha kampuni ya Jagro Enterprises Limited yenye makao makuu yake jijini mbeya wakiendelea na shughuli ya ushushaji wa moja ya mabango yaliwekwa katika ubao wa matangazo wa Continental katika eneo la stendi kuu ya mabasi jijini Mbeya.

Kazi ya ushushaji mabango ikiendelea





Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Jagro Limitted, leo imeshusha mabango ya matangazo yanayomilikiwa na Kampuni ya Continental yenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam, baada ya kushindwa kulipa ushuru wa zaidi ya milioni 100 kwa halmashauri ya Jiji la Mbeya.


Kiasi hicho cha fedha ni malipo ya ushuru katika mwaka wa fedha wa 2014 na 2015, ambapo Kampuni hiyo ya Continental ikiwa na dhamana ya kutangaza matangazo ya biashara kutoka kwenye mashirika na makampuni  mbalimbali kwa kutumia nguzo za mabango ya chuma.


Akizungumza na waandishi wa habari, leo katika eneo la tukio la stendi kuu ambapo zoezi hilo lilikuwa likifanyika, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jagro, Maulid Khamis, anasema  kampuni hiyo inatekeleza agizo la halmashauri ya Jiji laMbeya linalowataka kuyashusha mabango ya matangazo ya biashara kutokana na wahusika kushindwa kulipa kodi kama sheria ndogo za halmashauri zinavyowataka.


Amesema, kwa mujibu wa sheria ndogo ya halmashauri ya Jiji la Mbeya ya mwaka 2014 na sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 2012 inayowataka wamilikki wa matangazo kulipia matangazo hayo kwa kuzingatia sheria ndogo zinazopitishwa na halmashauri husika.


Anasema, kutokana na sheria hizo kukiukwa, halmashauri imetoa kibali kwa kampuni ya Jagro kuyashusha mabango hayo ikiwa ni moja ya majukumu waliyoingia mkataba na halmashauri hiyo ya Jiji la Mbeya.


Akizungumzia hilo,Mwanasheria wa Kampuni hiyo ya Jagro, Aloyce Mrema, anasema mbali na mabango hayo kushushwa pia wamiliki watafikishwa mahakamani .
Mwisho.




Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top