Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limemteua Baraka Kizuguto kuwa Ofisa Habari kuanzia
Februari 1 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo,
Kizuguto alikuwa Ofisa Habari wa klabu ya Young Africans, nafasi aliyoitumikia
kwa miaka miwili.
Kizuguto ana Stashahada
ya Juu ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha LEARN IT cha Dar es Salaam. Pia
ana ujuzi wa kusanifu tovuti, ufundi wa kompyuta na uchambuzi wa mifumo ya
kompyuta.
Mei mwaka jana, Kizuguto
aliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhudhuria
mafunzo ya usajili na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao
(TMS) yaliyofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.
TFF inamtakia kila la
kheri katika majukumu yake mapya.







Post a Comment