Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limeukomboa mji wa Baga, kaskazini mashariki mwa nchi ambako mamia ya watu waliuliwa na kundi la Boko Haram mwezi uliopita.
Jeshi lilisema kumetokea mapambano makali na wapiganaji hao Waislamu na hasara ilikuwa kubwa.
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, lilisema kuwa watu kama 2,000 waliuwawa Boko Haram ilipoiteka Baga - shambulio lao kubwa kabisa.
Serikali ya Nigeria ilisema watu 150 walikufa katika mji huo.
Baga iko kando ya Ziwa Chad kwenye jimbo la Borno - Boko Haram waliposhambulia maelfu ya watu walivuka ziwa kutafuta hifadhi nchini Chad.BBC

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top