Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi.


Na Emanuel Madafa,Mbeya
Vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto vimeendelea kushika kasi licha serikali na mashirika mbalimbali na haki za binadamu  kupiga vita vitendo hivyo kwa nguvu vimeendelea kujitokeza tena mkoani hapa.

Hali imejitokeza katika kijiji cha Iwezi Mbozi   pamoja na Ilolo jijini Mbeya.

Katika tukio la kwanza Mkazi wa Mtaa wa Ilolo jijini Mbeya Ndugu Gwandumbi Kipenya (32) amemuua Mke wake kwa kumpiga nondo kichwani Ndugu Zainabu Gwandumbi [29]  kisha na yeye kujiua kwa kujinyonga .

 Tukio hilo lilitokea  Feb 08 mwaka huu majira ya saa 09:00 usiku katika mtaa wa ilolo,kata ya sinde, jijini mbeya ambapo inadaiwa  kuwa . Mara baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa Gwandumbi kipenya aliingia chumbani na kujinyonga kwa kutumia mkanda wa begi hadi kufa.

Hata hivyo Chanzo cha matukio hayo  bado kufahamika kwani hakuna ujumbe wowote uliokutwa ndani ya nyumba hiyo.


Wakati huo huo jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Iwezi Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya Ndugu Saidia   Laison Mbagwa [65], baada ya kumfungia ndani ya nyumba mtoto wake ambaye ni mlemavu.

Tukio hilo lilitokea Feb 08 mwaka  majira ya saa 16:00 jioni  katika kijiji cha iwezi,kata ya igamba Wilayani Mbozi.

 Katika tukio hilo mhanga ambaye ana matatizo ya akili na kuanguka ugonjwa wa kifafa, alikutwa amefungwa kamba miguuni na kunyanyapaliwa kwa kufungiwa chumba maalum kwa muda wa miezi miwili  hivyo kupelekea  kudhoofu afya na kupelekwa hospitali ya serikali wilaya ya mbozi kwa matibabu.

 Mtuhumiwa baba mzazi wa mhanga amekamatwa na taratibu zinafanywa ili afikishwe mahakamani.

Aidha kamanda msangi anatoa wito  kwa jamii   hususani wanandoa kutatua matatizo/kero/migogoro yao kwa njia ya mazungumzo badala ya kujichukulia sheria mkononi kwani inaleta madhara makubwa kwa jamii na hususani familia.
MWISHO.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top