Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi katika Zahanati ya Kijiji cha Kimondo Kata ya Igoma Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika moja miradi ambayo Waziri Mkuu ametembelea katika ziara yake Mkoani Mbeya Feb 26 Mwaka huu.




Nyumba za watumishi katika zahanati hiyo ya  kijiji cha kimondo Kata ya Igoma Halmashauri ya Mbeya vijijini ambapo nyumba hizo zinauwezo wa kuishi familia 2 ambapo mradi huo kwa ujumla unatalajiwa kugahrimu zaidi ya shilingi mil74 huku serikali kuu ichangia shilingi mil 51.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kimondo Kata ya Igoma Halmashauri ya Mbeya vijijini mara baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji wa jiwe la msangi katika zahanati ya kijiji hicho feb 26 mwaka huu.

Mkurugenzi Halmashauri ya Mbeya vijijini Ndugu Upendo Sanga akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi wa kwanza kulia akiwa eneo la tukio kuhakikisha ulinzi unaimalika .
Wananchi wakifatilia hotuba ya Mheshimiwa Wazri Mkuu Mizengo Pinda .


Jamiimoja blog

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top