Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Moja ya mjadala ambao umechukua nafasi kubwa leo mitandaoni ni kuhusu ishu ya uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kuhusu kesi iliyofugiliwa na Mbunge Zitto Kabwe. Taarifa iliyoenea mitandaoni na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari inasema Mahakama imetupilia mbali kesi ambayo ilifunguliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuhusu kujadiliwa uanachama wake ndani ya chama hicho, ambapo katika hukumu hiyo Zitto ametakiwa pia kulipa gharama zote za kuendesha kesi hiyo. 

Zitto Kabwe amepata nafasi ya kuongelea hilo>>‘Mimi nilikuwa kwenye kikao cha Mamlaka ya EWURA nikajulishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kesi yetu imetupwa’ ‘Lakini kwenye kumbukumbu zetu ilikuwa twende Mahakamani tarehe 12 mwezi wa 3 sio kwa ajili ya maamuzi ni kwa ajili ya kesi kutajwa, kwetu sisi tumeshangazwa kwamba kesi imefanyika leo kwa maamuzi kesi ambayo ilipaswa itajwe vile vile siku hiyo hiyo Chadema kutangaza kwamba wamenivua uanachama mimi mpaka sasa sina taarifa rasmi na naendelea na kazi zangu kama kawaida’ Kwenye sentensi nyingine Zitto Kabwe amesema; ‘leo nilikua na EWURA.. ratiba yangu inaonyesha kesho nitakuwa na TANESCo na keshokutwa nitakuwa nashughulikia mabilioni ya Uswisi’ ‘Kwa upande wangu mimi taarifa yoyote rasmi sina, nitaweza kusema chochote baada ya kupata taarifa rasmi.. Wanasheria wangu wamekwenda Mahakamani kwa ajili ya kupata hiyo Judgement na kuweza kuona hatua gani zitakazofuata katika hiyo 
Judgement’– Zitto Kabwe. Bonyeza play kumsikiliza Zitto Kabwe. Credit Millard Ayo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top