Majonzi |
Baba wa marehemu |
Sehemu ambayo inadaiwa kuibiwa mbuzi huyo |
MTU mmoja amepoteza maisha
baada ya kupigwa na mtu au watu wasiojulikana na miguuni kwake kukiwa
kumefungwa mbuzi aliye hai katika eneo la Nsalala Kata ya Mbalizi Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya Nyagesa Wankyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja marehemu
kuwa ni Robart Mwasenga (35) ambaye aliuawa juzi usiku baada ya kupigwa na mtu
au watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi.
Inadaiwa kwamba kuwa
Marehemu huyo kabla ya kufikwa na mauti alifika kwenye banda la mifugo
linalomilikiwa na Wilison Mwangasani ambaye ni jirani yake na kutaka kuiba
mbuzi .
Akizungumzia tukio hilo Mtendaji
wa Kitongoji cha Nsalala Lwitiko Mwaibindi, amesema alipata taarifa kutoka kwa
raia mwema, kwamba kuna mtu anahitaji msaada wa haraka kwani anaonekana
amepigwa na kuumizwa.
“Baada ya kupokea taarifa
hii, nilifikisha ujumbe kwa mwenyekiti wa Kitongoji Stephano Mshani ambaye alifika na kumkuta kijana huyo akiwa
katika hali mbaya kutokana na kipigo alichopata,”amesema.
Amesema badaa ya kuona hali
hiyo alilazimika kukimbia hadi kituo cha polisi kwa lengo la kutoa taaraifa
hizo majira ya saa 5 usiku ambapo hata hivyo alikuta kituo kimefungwa kwa muda
huo.
Amesema baada ya kutumia
jitihada binafsi kwa kugonga mlango hatimaye alifunguliwa na mmoja wa askari baada
ya dakika 15 tangu afike kituoni hapo na kupokewa kwa kauli za vitisho toka kwa
askari huyo ambaye hakuwa tayari kumtaja jina akidai kuwa mwenyekiti huyo
amekiuka taratibu kwani muda wa kazi huishia saa 4 usiku hivyo alipaswa kufika
asubuhi.
Aidha baada ya askari
kumtaka mwenyekiti kurudi kesho yake hali ilibadilika ambapo kulitokea
majibizano yaliyopelekea mwenyekiti kuwekwa mahabusu hadi saa 8 mchana siku
iliyofuata.
Amesema kitendo cha yeye
kuwekwa mahabusu pamoja na askari kushindwa kufika eneo la tukio kwa muda huo kumechangia
kwa kiasi kikubwa marehemu kupoteza maisha kwani kulikuwa na uwezekano wa
kupona endapo angewahishwa hospitali.
Hata hivyo baada ya sakata
hilo kati ya polisi na mwenyekiti,
hatimaye mtendaji wa kitongoji alilazimika kufika kituo cha polisi na
kumuwekea mzamana mwenyekiti wake majira ya saa 8 chana .
Akijibu tuhuma hizo,Kaimu
kamanda wa polisi Mkoa wa mbeya Bw. Nyigesa Wankyo amekiri kupokea taarifa hizo
na kuahidi kuzifanyia kazi lakini mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi na
kukabidhiwa kwa ndugu zake tayari kwa maziko.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment