Timu za Kiluvya United ya Pwani, Mbao FC ya jijini Mwanza,
Mji Njombe kutoka mkoa mpya wa Njombe na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma zimepanda
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuongoza katika misimamo ya makundi yao ya
Ligi Daraja la Pili (SDL).
Kwa kuzingatia Kanuni ya 5 (8) ya Ligi Daraja 9SDL Toleo la
2014, hatua ya pili Ligi Daraja la Pili kutafuta Bingwa na sasa timu hizo zitacheza
kusaka Bingwa wa ligi Daraja la Pili.
Mji Njombe itacheza na timu ya Kiluvya United tarehe 14
Machi mwaka huu katika uwanja wa Amani Makambako, na mchezo wa marudiano
kufanyika tarehe 18 Machi, 2015 katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Nayo Mbao FC ya Mwanza watawakaribisha timu ya Mji Mkuu FC
mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na mechi ya
marudiano itachezwa Machi 18, 2015 katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Fainali inatarajiwa kufanyika Machi 22 mwaka huu jijin Dar
es salaam (uwanja wa mchezo utatangazwa baadae) kwa kuzikutanisha timu
zilizopata pointi nyingi katika michezo hiyo miwili ya awali.
Post a Comment