![]() |
| Polisi waliogundua maiti hizo wakishika doria nje ya nyumba hiyo |
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kufuatia mauaji ya wanawe wawili waliopatikana wamefungikiwa ndani ya jokofu.
Maafisa
wa polisi wanasema kuwa mwanamke huyo mama wa watoto wanne
aliwatumbukiza wanawe wawili wenye umri wa miaka 11 na mwengine mwenye
umri wa miaka 14 ndani ya jokofu baada ya kuwaua.
Aidha miili ya mvulana 11, na msichana 14, ilipatikana imewekwa kwenye karatasi za plastiki ilizisivunde.
Yamkini
miili hiyo ilipatikana na maafisa wa idara ya mahakama waliokwenda
nyumbani kwa mama huyo kwa nia ya kumfurusha baada ya kushindwa
kugharamia kodi ya nyumba .
Walishtuka kupata miili ya watoto hao na mara moja wakawaarifu maafisa wa polisi katika jimbo hilo.
Wanawe wawili waliosalia walikuwa kwa jirani na walichukuliwa na kupewa usalama.
Uchunguzi na upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanyika ilikubaina kiini haswa cha vifo vyao.
Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo James Craig ametaja kitendo cha mwanamke huyo kuwa cha kuogofya mno.
Jirani
ya mwanamke huyo Tori Childs, aliliambia shirika la habari la AP kuwa
watoto hao wawili waliopatikana walikuwa wametoweka kwa takriban mwaka
mzima .
Majirani wengine walisema kuwa mwanamke huyo alikuwa
taabani haswa baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba, na kuwa mama
huyo mwenye umri wa
miaka 36 alikuwa kanakwamba anakabiliwa na upungufu fulani maishani mwake.







Post a Comment