Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na Omary Katanga,Dar es salaam

Baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na timu za FFU na Zakhem kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao,kesho 20/03/2015 utapigwa mchezo mmoja wa kusaka nafasi ya kuungana na mabingwa hao kushiriki michuano ya ligi ya mikoa.
Mchezo huo wa mtoano utakaopigwa katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,utazikutanisha timu za Pan Africa dhidi ya Changanyikeni ambazo zimemaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam,DRFA,baada ya kumpata mshindi katika mchezo huo, majina ya timu hizo tatu yatapelekwa shirikisho la soka la Tanzania TFF.
Aidha kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Kenny Mwaisabula,imewashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja mbalimbali kushuhudua michuano ya ligi mkoa wa Dar es salam tangu ilipoanza kutimua vumbi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top