Na Mwandishi Maalum.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon, amesema kama si utashi wa
kisiasa, kujituma, na kujitolea kulikofanywa na viongozi mbalimbali
aliowaomba kufanya naye kazi kwa karibu huku wengine wakijitolea
wenyewe, uhai wa wanawake na watoto 2.4 milioni usingeokolewa.
Ban Ki
Moon ameyasema hayo siku ya Jummane wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya
kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la kila mwananamke, kile
mtoto, ( every woman, every child) mkakati ambao Ban Ki Moon
aliuratibu mwaka 2010 .
“ Siri
kubwa ya mafanikio ya mkakati huu ni uwajibikaji. Nilipoanzisha
mkakati huu niliwaomba baadhi ya viongozi wanisaidie, wapo waliosaidia
katika uhamasishaji wa raslimali fedha, wapo kama Rais Jakaya Kikwete
wa Tanzania na waziri Mkuu wa Canada ambao walisimamia suala zima la
habari na uwajibikaji, mchango wao, kujituma kwao na uthubutu wao
ndiyo umetufikisha hapa , tumeweza kuokoa maisha ya wanawake na watoto
wengi na kazi bado inaendelea” ameeleza Katibu Mkuu.
Akasema
mkakati huo aliouzisha wa kila mwanamke, kila mtoto na ambao
chimbuko lake ni lengo namba nne na tano la maendeleo ya millennia ni
mkakati ambao si tu umekuwa wa mafanikio makubwa lakini umegusa
hisia za wadau mbalimbali za watu wengi .
Malengo
namba nne na tano ya maendeleo ya millennia na ambayo yanafikia
ukingoni mwisho mwa mwaka huu yanajikita katika kupunguza idaidi ya
vifo vya wanawake na idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
“Nilianzisha
mkakati huu kwa sababu mimi mwenyewe nimeguswa katika maisha yangu
utoto wangu kwa kuondokewa( kufariki) kwa kaka na dada zangu kwa
matatizo ambayo yangeweza kuzuilika. Simulizi alizokuwa akisimuliwa na
mama yake juu hofu kuu wanayokuwa nayo wanawake wanapokwenda
kujifungua vile vile ni moja ya hamasa iliyonifanya nianzishe mkakati
huu. Lakini pia katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na visa
vingi vilivyoongea nia na ari kuwa na mkakati huu” ameeleza Ban Ki
Moon.
Ripoti
hiyo ambayo uzinduzi wake umekwenda sambamba na mkutano wa 59 wa
Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake, inabainisha kwa kina mafanikio na
changamoto mbalimbali za utekelezaji wa katika eneo hilo linalohusu
afya ya mama na mtoto.
Ban Ki Moon amesema amefarijika na kutiwa moyo sana
Kwa
mfano Makati huo ambao umegusa hisia wa wadu mbalimali wakiwamo
viongozi wakuu wan chi na serikali, asasi zisizo za kiraia,
wanaharakati na makampuni binafsi.
taarif
yasingeushirikiano wa karibu baina yake na Viongozi wakuu wa mataifa
mbalimbali umesaidia kuokoa maisha ya …………….., ambao wangepoteza maisha
yao wakati wa kujifungua.
Post a Comment