|
Wakazi wa eneo la mtaa wa Mwambenja Isanga jijini mbeya wakimsubiri Mtendaji wa Mtaa wa Mwambenja Kata ya Iganzo Jijini Mbeya Alex
Luvanda kwa lengo la kutaka ufafanuzi juu ya kero mbalimbali zinazo wakabili waka zi hao ikiwemo suala la vitendo vya rushwa pindi wanapohitaji huduma ofisini kwake. |
|
Mtendaji wa Mtaa Mwambenja Kata ya Iganzo Jijini Mbeya Alex
Luvanda akiwasili eneo la tukio kujibu hoja za wananchi wake mara baada ya kumtuhumu
kwa vitendo vya rushwa pindi wanapohitaji huduma ofisini kwake. |
|
Diwani kata ya Mwambenja Uswege Fulika akiwasihi wananchi hao kuto fanya vurugu |
|
Mtendaji akizongwa na wananchi |
|
Kichapo |
|
Kichapo |
|
Mtendaji akitimua baada ya mshikemshike |
Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya
Mtendaji
wa Mtaa wa Mtaa wa Mwambenja Kata ya Iganzo Jijini Mbeya Alex Luvanda
amenusurika kipigo kutokwa kwa wakazi wa Mtaa huo wakimtuhumu kwa
vitendo vya rushwa pindi wanapohitaji huduma ofisini kwake.
Majira
ya saa mbili asubuhi Machi 9 mwaka huu wananchi walimtaka Diwani wa
Kata hiyo Uswege Fulika kufika katika ofisi ya Mtendaji wa Mtaa ili
kupokea malalamiko yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya Mtendaji
huyo vya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Baada ya
Diwani kufika eneo hilo wananchi waliokuwa na ghadhabu hawakutaka
mkutano tena badala yake walimwamuru Diwani kufungua ofisi ya Mtendaji
ili Mtendaji achukue vifaa vyake aondoke Mtaani hapo kutokana na vitendo
vya manyanyaso.
Wananchi hao wakiongea kwa mukali mkubwa
walimwambia Mtendaji amekuwa akiwatoza fedha wananchi hao kati ya
shilingi elfu thelathini hadi milioni moja bila kutoa stakabadhi yoyote
hali iliyozua manun'guniko ya mara kwa mara.
Vurugu
zilipoanza kushamiri Diwani alilazimika kufanya kazi ya ziada kumnusuru
Mtendaji kwa kumtaka kuondoka eneo hilo kwa kutumia pikipiki yake hadi
katika ofisi ya Kata huku akisindikizwa kwa maneno na wakazi hao wakimta
Diwani kuhakikisha Mtendaji huyo harudi mtaani hapo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwambenja Lucas Mwakalonge amesema
kuwa Mtendaji huyo amekuwa akifanya kazi peke yake bila kushirikisha
kamati ya Mtaa hali iliyozua malalamiko kwa wananchi.
Mwakalonge
baada ya kushindwa kuhimili malalamiko hayo alimuomba Diwani kufika
Mtaani hapo ili apokee kero za wananchi ambapo Diwani alifika lakini
alishindwa kutimiza azma yake kutokana na jazba za wananchi waliomwamuru
Mtendaji kuondoka mara moja kutokana na kuchoshwa na vitendo vya
Mtendaji wao.
Hata hivyo baada ya kuona mambo yanamwendea
kombo Mtendaji aliita kinyemela Askari wa kituo kikuu cha kati kwa madai
kuwa kuna Mwananchi mmoja wa Mtaa huo amemjeruhi mtoto sikio hivyo
Polisi waje ili achukuliwe hatua za kisheria.
Baadhi ya
wananchi hao walidai suala hilo kupelekwa Polisi ni pale ambapo
mtuhumiwa aligoma kutoa kitita cha shilingi milioni moja kwa watoto
wawili ambao ilidaiwa kuwa hawendi shule.
Polisi waliamua
suala hilo kulikabidhi katika Dawati la Jinsia ili kulishughilikia
kikamilifu na kurudisha amani katika Mtaa huo.
Diwani
Uswege Fulika amesema Mtendaji huyo amehamishiwa katika Mtaa huo
amehamishiwa katika mtaa huo miezi mitatu iliyopita hivyo kutokana na
mtafaruku huo amesema ataitisha kikao cha dharua cha Kata ili
kumwandikia Mkurugenzi wa Jiji ambaye ni Mwajiri wa Mtendaji huyo ili
amhamishi katika Kata hiyo kuokana na Mtendaji huyo kushindwa kutimiza
majukumu yake.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment