Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.
 wanafunzi wakifuatilia hotuba za uzinduzi kutoka kwa viongozi.
Mgeni rasmi pamoja na meza Kuu ikipiga picha na Vilabu mbalimbali kutoka shule za sekondari na msingi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa klabu za wanafunzi watumiaji wa huduma za usafiri mkoa wa Dar es salaam jana. Wengine ni  Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano na Mwenyekiti wa Baraza hilo Ayoob Omary. Picha na Sori: mrokim.blogspot.com
Na Father Kidevu Blog
BARAZA la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), limezindua klabu ya wanafunzi ijulikanayo kama “Sumatra Club” jijini Dar es Salaam.

Sumatra Club itakuwa inatoa mafunzo na mbinu zitakazowawezesha wananfunzi kutambua haki zao katika huduma ya usafiri nchini huku kauli mbiu yao ikiwa inasema, “Mtetezi wa haki, maslahi na wajibu wa abiria”.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya sabasaba, Mwenyekiti wa Baraza hilo,  Ayoob Omary amesema kuanzishwa kwa vilabu vya Sumatra mashuleni kutasaidia kutoa elimu kwa wanafunzi ili wajue haki zao katika huduma ya usafiri.

“Sumatra imeamua kuanzisha vilabu hivi mashuleni ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi watambue haki zao katika huduma ya usafiri na wajue namna ya kutatua matatizo wanayokumbana nayo katika vyombo vya usafiri,” alisema Omar.

Sumatra Club vimesha zinduliwa katika mikoa ya tisa nchini, miongoni mwayo ni pamoja na Mbeya, Mwanza, Mtwara na Dar es Salaam na tayari wanafunzi wake wamenza kupatiwa mafunzo hayo ya haki ya mtumiaji wa vyombo vya usafiri nchi kavu na majini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo amesema mara nyingi watumiaji huduma za usafiri wamekuwa wakinung’unika ilhali wanapaswa kulalamika maana manung’uniko hayafiki popote.

“Wanafunzi nimiongoni mwa wadau na watumiaji wakubwa wa usafiri hasa wan chi kavu na wamekuwa wanung’unikaji wakubwa  kwa muda mrefu lakini sasa tunataka wawe walalamikaji kwa kufuata sheria na haki walizonazo katika huduma za usafiri,Alisema Kikoyo.

Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na Sumatra pamoja na wanafunzi wenyewe wataweza kumaliza changamoto ya usafiri kwa wanafunzi kama vilabu hivi vitasimamiwa vizuri.

“Tatizo la usafiri kwa wanafunzi litapungua na kuisha iwapo tutasimamia vyema vilabu vyetu. Niwaombe wanafunzi wawe waadilifu na watiifu wa sheria, msiwe chanzo cha vurugu kwenye vyombo vya usafiri. Kuweni watatuzi wa matatizo,” alisema Kahatamo.

Uanzishwaji wa vilabu hivi imeelezwa kuwa ni moja ya mbinu iliyobuniwa na baraza la hilo ili kukabiliana na changamoto ya usafiri kwa wanafunzi. Kila mkoa utakuwa na vilabu vyake vya Sumatra kwa utaratibu utakaowekwa na mikoa husika.

Mathias Kondrad mwanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Kibasila amesema, “Nimefurahi sana kuanzishwa kwa vilabu hivi, tunaimani nasi sasa tutathaminiwa kama abiria wengine. Tumekuwa tukichelewa shule kwa kukataliwa na hata kupigwa na makondakta ili tusipande magari yao. Lakini sasa hivi tutatumia sheria kudai haki yetu ya msingi kama abiria,” alisema Kondrad.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top