Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mbeya moja wakiangalia mahindi yaliyofyekwa na wananchi wa kijiji cha ndaga kwa madai ya kutengeneza barabara .Picha na Ezekiel Kamanga




Baadhi ya wananchi wakiwa wameshika miche ya mahindi iliyofyekwa na wakazi wa ndaga kwa lengo la kutaka kupitisha barabara katika eneo hilo

Diwani kata ya Isongole( katikati) Bw.Laurence Nyasa akiwa pamoja na wananchi wake akiangalia uharibifu mkubwa uliyofanywa na wananchi wa ndaga Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.




Mwenyekiti wa kijiji cha Mbeya Moja Chesko Jafary akiwa katika moja ya mashamba yaliyoharibiwa na wananchi wa ndaga ambao wamefanya uhalibifu huo kwa lengo la kutaka kupitisha barabara bila ridhaa ya wahusika .

Wananchi wa kijiji cha Mbeya Moja wakiwa katika mkutnao wa hadhara ili kupata suluhisho juu ya uharibifu huo.


Mwenyekiti wa kijiji akihutubia wananchi
Mkutano ukiendelea

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya
Wananchi wa Kijiji cha Mbeya Moja  Kata ya Isongole na Kata ya Ndaga wameingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya wananchi wa Ndaga kufyeka mahindi bila ridhaa ya wananchi wa Isongole kwa madai ya kupata barabara ya kupitishia mazao kutoka shambani.

Tukio hilo la aina yake limetokea Februari 26 mwaka huu baada ya mkazi mmoja wa Ndaga ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji kuamuru wananchi wake kufyeka mahindi umbali wa kilomita zaidi ya moja bila kujali mahindi yamekomaa au la na baadhi ya wananchi kuondoka nayo.

Baada ya kupata taarifa za mahindi kufyekwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbeya 1 Chesco Japhary alikwenda na kushuhudia uharibifu mkubwa uliofanywa na wananchi wa Ndaga Mwenyekiti alitoa taarifa kwa Diwani wa Kata ya Isongole Lawrence Nyassa.

Diwani baada ya kukagua mashamba hayo alimshauri Mwenyekiti kutoa taarifa Polisi Kituo cha Kiwira ambapo baada ya kuona ukubwa wa tukio waliwaamuru Viongozi wa Isongole kwenda kutoa taarifa kituo kikuu cha Rungwe ili watuhumiwa wakamatwe na kujibu tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo mpaka sasa Jeshi la Polisi halijamkamata kinara wa uharibifu kwa kile kinachodaiwa kuwa yeye hawezi kukamatwa na mtu yeyote na kwamba hili si tukio la kwanza kulifanya katika Vijiji jirani vinavyopakana na Vijiji vya Ndaga.

Hivi karibuni wananchi wa Ndaka walichoma hifadhi ya msitu wa Isongole na kufanya uharibifu mkubwa hali iliyofanya wananchi kufanya juhudi za ziada kuokoa msitu huo usiteketee kabisa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Isongole Lawrence Nyassa amewataka wananchi wake kuwa na subira badala ya kujichukulia sheria mkononi na pia amekerwa na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na wananchi wa Ndaga mara kwa mara na tukio hili ni la tatu katika utawala wake.

Vitendo vingine ni pamoja uchomaji wa msitu,kun'goa mazao hususani viazi kwa madai ya kuchimba mtaro wa maji na sasa kufyekwa kwa mahindi.

Pamoja na uharibifu wote huo hakuna fidia yoyote waliyopewa wananchi wa Isongole licha ya gharama kubwa ya mbolea na pembejeo za kilimo walizotumia ikiwa ni pamoja na mbolea za ruzuku hivyo kukwamisha juhudi za serikali za kuondokana na njaa na kukuza uchumi.

Mwenyekiti wa Kijiji alimwagiza Afisa ugani Felisia Mbuna kukagua mashamba yote ili kubaini thamani halisi ya hasara iliyopatikana ili kila hanga alipwe fidia yake.

Kutokana na adha hiyo Kijiji kilifanya mkutano wa hadhara Machi 4 mwaka huu ili kupata mustakabali wa suala hili.



                                                                     Mwisho.




                                                           JAMIIMOJABLOG



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top