Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Moja ya gari lililotumika kuingiza bidhaa halamu kupitia nchi za panya


Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya anayeshughulika  na Forodha Ndugu Joseph Ruge akizungumza na waandishi wa habari katika eneno la uteketezaji wa bidhaa hizo eneo la Nsalaga Uyole jijini Mbeya.

Mkaguzi wa chakula na Dawa kanda ya Nyanda za juu kusini (TFDA) Ndugu Yusto Wallece

Afisa Mfawidhi Forodha Kituo cha Mbeya Ndugu Magaty Gendo

Uteketezaji ukiendelea katika eneo la Dampo Nsalaga Uyole jijini Mbeya





Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Chakaula na Dawa (TFDA) Kanda ya Mbeya  imeteketeza bidhaa halamu zilizoingizwa nchi bila kibali kupitia mipaka ya Tunduma ,Malawi,kongo.


 Bidhaa hizo ni pamoja na Pombe kali aina ya Viloba  katoni 3000 ,mifuko bandia kwa ajiri ya upakiaji wa sukari , Juice ambazo zimekwisha muda wake katoni 26  ambapo kwa pamoja mzigo wote ukiwa na gharama ya shilingi mil 4 na laki 7.


Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya anayeshughulika  na Forodha Ndugu Joseph Ruge amesema bidhaa hizo zimetoka katika nchi za jirani ambazo ia ni Malawi.Zambia pamoja na Kongo kwa kupitia njia za panya.

Amesema ukamataji wa bidhaa hizo unatokana na ushirikiano na taasisi mbalimbali likiwemo jeshi la Polisi Mkoani humo pamoja na wadhibiti wa chakula na dawa TFDA na wadau wengine .


Amesema katika uteketezaji wa bidhaa hizo umegawanyika katika maneneo tofauti ambapo zipo bidhaa ambazo zilikamatwa zikiwa sokoni ambazo muda wa matumizi yake ukiwa umekwisha pamoja na zile ambazo zimeingizwa nchi bila kibali maalumu kupitia njia za panya.

Kufuatia hali hiyo Meneja huyo ametoa wito kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wanannchi juu ya matumizi ya bidhaa ambazo zimekwisha muda wake .


Kwa upande wake Mkaguzi wa chakula na Dawa kanda ya Nyanda za juu kusini (TFDA) Ndugu Yusto Wallece amewataka wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza bidhaa hizo nchini kwa kuhakikisha wanafuata taratibu za uingizwaji wa bidhaa hizo nchini kwa lengo la kuepuka hasara hizo pamoja na kulinda afya za walaji .


Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanaingiza bidhaa zilizokidhi viwango kwa ajili ya matumizi ya binadamu badala ya kukimbilia faida ambayo italeta madhara kwa binadamu hususani  pombe halamu ambazo zimegharimu maisha ya vijana wengi katika mkoa wa mbeya na maeneno mengine..
                                                     
 Akizungumzia suala la ukamataji wa bidhaa hizo afisa forodha kituo cha Mbeya Ndugu Magaty Gendo amesema bidhaa hizo zimekuwa zikipitia njia za panya hivyo wao kama mamlaka watahakikisha wanaendeleza juhudi hizo kwa kufanya kazi usiku na mchana.              

  Mwisho
 JAMIIMOJABLOG

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top