Eneo ambalo ujenzi wa chuo hicho cha Veta kitajengwa |
Balozi Mdogo wa Japan Nchini Tanzania Ndugu Kazuyoshi Matsunag akizungumza na waandishi wa habari. |
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Janeth Mbene( kulia)akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndugu Rosemay Senyamule mara baada ya kutembelea eneo la mradi |
Mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemay Senyamule akimkabidhi zawadi Balozi wa Mdogo wa Japan Kazuyoshi Matsunaga mara baada ya kukamilisha zoezi la utiaji saini mkataba. |
Na Mwandishi wetu,Ileje
Ubalozi wa Japan nchini
Tanzania umesaini mkataba na halmashauri
ya Wilaya ya Ileje kwa ajili ya ujenzi wa
chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (Veta) katika
halmashauri hiyo ambao utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 100.6 za
Kitanzania.
Mkataba huo umesainiwa na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani mbeya Ndugu Mussa Otieno na
Balozi Mdogo wa Japani Ndugu Kazuyoshi Matsunaga katika ofisi za halmashauri
hiyo ya Ileje.
Akizungumza mara baada ya
kusaini Mkataba huo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndugu Mussa Otieno amesema
teyari wamekwisha pokea milioni 100.6 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mawili ambapo
malengo ilikuwa ni kujenga darasa miwili pamoja na karakanamoja hivyo msaada huo umelenga sehemu husika.
Amesema eneo ambalo litajengwa chuo hicho
linaukubwa wa hekari mbili na nusu hivyo
bado halmashauri hiyo ipo katika mkakati wa kuongeza ukubwa zaidi wa eneo hilo
ili kuweza kukidhi zaidi mahitaji ya ujenzi wa chuo hicho.
Vilele Otieno amesema kuwa
gharama halisi ya ujenzi huo bado haijafahamika hivyo mpango uliopo sasa ni
kukutana na watu wa Veta ili kupata halisi ya mahitaji ili kukamilisha ujenzi
huo.
Amesika endapo chuo hicho kitakamilika kitakuwa na
uwezo wa kuhudumia wilaya nzima ya Ileje pamoja na maeneo mengine ya jirani
hivyo msaada huo ni chachu kubwa ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Amesema ujenzi huo
unatalajiwa kuanza mapema mwaka huu ambapo hadi 2016 ujenzi huo utakuwa
umekamilika na chuo kuanza kutoa huduma .
Naye balozi Balozi mdogo wa
japan Ndugu Kazuyoshi Matsunaga amesema kutolewa kwa msaada huo kunatokana na
kuwepo kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya ubalozi wake na Naibu waziri wa Viwanda
na Biashara Janeth Mbene hivyo anaamini kuwa mchango huo utasukuma juhudi za
serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Balozi huyo amesema
kuwa ushirikiano wake na Tanzania utaendelea
kuimarika kwa kuhimiza maendeleo kwa pande zote mbili na amani ya watu wake.
Kwa upande wake Mheshimiwa
Janeth Mbene Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara amesema
mchakato huo umechukua kwa zaidi ya miaka miwili hadi kupatiwa msaada
huo na ubalozi wa japan hivyo kuwepo kwa
chuo hicho katika halmshauri ya Ileje ni hatua kubwa kwani wanafunzi wengi watakao maliza kidato cha nne
watapata fursa ya kuijunga na chuo hicho moja kwa moja .
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment