Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
CARDINAL PENGO


"Maaskofu Hatuna MAMLAKA Ya Kuwaamulia/Kuwalazimisha Waumini Wetu Wafanye Uamuzi Gani Kuhusu Katiba, Kuwaamulia ni Kuwadharau Kuwa Hawawezi Kufanya Uamuzi Sahihi Wao Wenyewe Na Kuingilia UHURU Wao.
WARAKA Huu Unaleta Utengano Katika Taifa Kuwa Wakristo Tumechukua Uamuzi Dhidi Ya Serikali Na Wengine....
Tuwaache Waumini Wafanye Uamuzi kwa Tafakari Yao Binafsi Bila Shinikizo Letu.....
Wakati Hili Linajadiliwa Nilikuwa ITALY Katika Kusimikwa Makardinali Na Baadaye India, Wengine Wakavumisha Nimelazwa,..Wengine Nimefariki, Lakini Namshukuru Mungu Hizo ni Dua ZA Kuniongezea Maisha Marefu Na Afya(Makofi)
Nililetewa Waraka Nikausoma, Umepitishwa Baada Ya Tafakari Kubwa Nauheshimu.
Lakini Nadhani Tuwaache Waumini Wafanye Uamuzi kwa UHURU Baada Ya Kutafakari....
Si Sahihi Tukaenda Katika Katiba Kama Wakristo kwa Shinikizo a kupinga KATIBA...
Wawe Huru Anayepinga kwa Hiari Yake Anayekubali kwa Dhamiri Yake....
Sidhani Kama Viongozi wa Dini Sasa Tuna Amri Ya Kulazimisha Uamuzi Juu Ya Katiba...."
CARDINAL PENGO LEO HII ST JOSEPH MISA YA WAWATA
KIONGOZI Makini Na Mwenye Busara Saana.
Hivi Kila Dini Ikianza Kuchukua Misimamo Kuhusu Mambo Ya KISIASA TANZANIA ITABAKI????

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top