Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Mtoto wa miaka (05) Jonson Mwamwere,
mkazi wa Nsalaga jijini mbeya, ameuawa kwa kupigwa sululu kichwani na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na mjomba wake Yona Mwamwere (38) Mkazi wa Nsalaga.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Machi 16
mwaka huu majira ya saa 11:00 asubuhi huko katika mtaa wa Nsalaga-Uyole,
Kata ya Nsalaga,jiji na Mbeya.
Awali inadaiwa kuwa, Yona Mwamwere alikuwa anamfukuza mtoto huyo ambaye ni mjomba wake
kutoka nyumbani na alikimbilia kwenye jengo lililopo jirani na nyumbani kwao
ambalo bado lipo kwenye ujenzi.
Hata hivyo taarifa zinadai kuwa, yona mwamwere alipofika kwenye jengo
hilo aliwatishia mafundi waliokuwa wanajenga na wote walikimbia, hivyo alimuua
mjomba wake huyo kwa kumpiga kichwani kwa sululu na kutenganisha kichwa na
kiwiliwili.
Kufuatia tukio hilo mafundi waliokuwa
wakiendelea na ujenzi walipiga kelele za kuomba msaada, hivyo kundi la wananchi
walioamua kujichukulia sheria mkononi walijitokeza na kumshambulia mtuhumiwa
kwa kumpiga hadi kufa na kisha kuuchoma moto mwili wake.
Marehemu wote walikuwa ni ndugu wanaoishi
nyumba moja, miili yao imehifadhiwa hospitali ya rufaa mbeya. Chanzo cha tukio
hili kinachunguzwa ingawa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu yona mwamwere alikuwa na matatizo ya
akili.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna
msaidizi mwandamizi wa polisiAhmed Msangi anatoa pole kwa familia ya marehemu
kutokana na tukio hilo.
Aidha anatoa wito kwa jamii/wananchi kuacha
tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake
wajenge tabia ya kuwafikisha katika mamlaka husika watuhumiwa wanaowakamata kwa
tuhuma mbalimbali kwa hatua zaidi za kisheria.
MWISHO
Jamiimojablog
Jamiimojablog
Post a Comment