na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA/CCC )
Hawa Ng’umbi
- See more at: http://jamiimoja.blogspot.com/2015/03/habari-picha-uzinduzi-wa-vilabu-vya.html#sthash.67ffRMCW.dpuf
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri kwa
watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA/CCC ) Hawa Ng’umbi akizungumza katika
mkutano huo
|
Wadau na waalikwa katika mkutano huo wakiwa makini kusikiliza mgeni rasmi. |
Mkutano ukiendelea |
Picha ya pamoja na meza kuu. |
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA zinazodhibiti ubora wa vyakula nchini,zimetakiwa
kufanya kazi kwa kushirikiana na kampuni za mawasiliano kwa kutumia fursa ya
teknolojia ya mawasiliano ili kuhakikisha kuwa haki za watumiaji wa vyakula
zinalindwa na huduma bora zinapatikana.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe
Munasa, wakati akifungua maadhimisho ya
Kitaifa ya wiki ya haki za mlaji na mtumiaji wa bidhaa Duniani ambapo kitaifa yanafanyika Mkoani
Mbeya, kupitia jukwaa la watumiaji kwa kushirikiana na mamlaka za mawasiliano
na mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji wanchi kavu na majini(SUMATRA).
Amesemaa, wafanyabiashara wa vyakula pamoja na kampuni za
kuhifadhi, kusindika na kusafirisha vyakula zinatakiwa kuhakikisha kuwa
zinatumia fursa zilizopo kulinda na kushajiisha matumizi ya teknolojia za
mawasiliano ili kulinda afya za watumiaji.
Amesisitiza kuwa nivema Mamlaka zinazodhibiti ubora wa
vyakula zikashirikiana kwa pamoja na
kampuni za mawasialiano kwa kutumia fursa ya teknolojia ya mawasiliano ili kuhakikisha
kuwa haki za mtumiaji wa vyakula zinalindwa na huduma bora zinapatikana.
Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wamehusisha suala zima la kutoa elimu
kwa watumiaji kuhusu wajibu na haki zao na kutoa tahadhari kwa watumiaji endapo
bidhaa zisizokidhi vigezo vya kuwepo sokoni zinapatikana.
Aidha, amesema kuwa kupitia maadhimisho hayo, watumiaji
wanapaswa kuzingatia zaidi matumizi ya vyakula asili, pale vinapokuwa na
urahisi wa kupatikana ili kupunguza kasi ya ongezeko la magonjwa ya kisukari,
kansa, mfumo wa damu nay ale yanayoathiri utendaji wa ufanisi wa moyo na figo.
Hata hivyo, Kiongozi huyo,alisisitiza kwamba hivi sasa
umefika muda muafaka kwa watumiaji kudai haki ya usalam wa chakula kwa kutoa
taarifa kwa mamlaka husika pale wana wa vyakula kutoka kwa watoa huduma.
Amesema ushiriki wa serikali katika maadhimisho hayo ni namna serikali inavyothamini na kuenzi majukumu muhimu yanoyotekelezwa na taasisi hizo hivyo serikali itaendelea kushirikiana katika kuboresha ufanisi na utendaji wa uchumi wa soko na kumlinda mtumiaji wa kitanzania.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya ya mbeya ameonyesha
kutoridhishwa na mwenendo wa utoaji wa huduma za matangazo katika vituo vya
radio na Tv kutokana matangazo mengi
kuto zingatia maadili sanjali na kiuka taratibu za utoaji huduma hiyo.
Kufuatia hali amezitaka taasisi husika kuangalia upaya
jambo hilo ili kutoa haki kwa mlaji na mtumiaji wa huduma hiyo .
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa pamoja na Tume ya ushindani (Fair Competitioni Commision)na baraza la ushauri kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa anga (TCAA,CCC) pamoja na baraza la ushauri kwa watumiaji wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Sumatra.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment