Mjumbe wa baraza kuu la Vijana Taifa Ndugu Neema Mdabila akizungumza na vijana hao. |
Vijana wakionyesha ukakamavu mbele ya Mwenyekiti wao . |
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Wilaya ya Ileje, John Mwinyisongole |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Ikiwa
imebaki miezi michache katika kuelekea
uchaguzi Mkuu mwezi Ocotba Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya, (UVCCM)
umewataka viongozi mbalimbali na wanachama wa chama hicho ambao wameonyesha nia
ya kugombea nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais , kuacha kuwagawa vijana kwa
maslahi yao binafsi kwa lengo la kujiuepusha na mpasuko na makundi miongoni
mwao.
Kauli
hiyo, imetolewa na Mwenyekiti wa Vijana
wa CCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, alipowatembelea baadhi ya vijana wa
chama hicho ambao wameweka kambi katika shule ya Msingi ya Itale iliyopo
Wilayani Ileje Mkoani Mbeya.
Amesema ,
hivi sasa wapo wanasiasa wenye kutaka nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia
ngazi za chini hadi juu kwa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais, hivyo wamekuwa
wakiwatumia vijana katika kufanikisha mambo yao hali ambayo imeanza kuonesha
kugawanyika kwa vijana hao.
Hata
hivyo, aliwataka baadhi ya wanachama ambao wameonyesha nia ya kutaka kushika
nafasi mbalimbali za uongozi, kutambua kuwa sababu ya chama cha mapinduzi
kuanzisha makambi hayo kwa vijana ni kutoa elimu, kuwajengea uwezo wa kisiasa
ili watambue majukumu yao.
Aidha
aliwataka vijana kuwa nguzo imara ya chama na kutumia mafunzo wanayoyapata kwa
ajili kuimarisha umoja na kuacha chuki miongoni mwao kwa masalhi ya chama cha Mapinduzi CCM..
Naye
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Wilaya ya Ileje, John Mwinyisongole,
aliwataka vijana wasikukubali kugawanywa kwa ajili ya fedha na kuwa imara
wakati wote na kuwataka kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika chaguzi
zinazokuja.
Hata hivyo
alisema UVCCM iko imara na hakuna mpasuko wowote na ndio maana kuna makambi
mbalimbali yanaendelea ndani ya jumuiya ua umoja wa vijana, na kwamba wako
imara na kwamba kama wapo ambao wanataka kuwagawa nafasi hiyo kwao haipo.
Mwisho.
Post a Comment