Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akiwahutubia washiriki wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa
na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere
jana Jijini Dar es Salaam na kuhusisha washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la
kuhamasisha matumizi ya lugha ya kiswahili.
![]() |
| Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz akizungumza na washiriki wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. |
Wanafunzi kutoka shule za Feza wakiburudisha wakati wa Tamasha la
Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na
kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam na kuhusisha
washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya lugha ya
kiswahili.Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo, CREDIT MICHUZI
Na Lorietha Laurence na May-Zuhura Simba -Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
ameeleza kuwa lugha ina mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa
itakuzwa sambamba na maendelao ya teknolojia.
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Kimataifa la
Lugha na Utamaduni na kufafanua kuwa tamasha hilo limeonyesha kukua kwa
lugha ya Kiswahili ambao ni utambulisho wa nchi yetu tangu kupatikana kwa
uhuru.
“Mkusanyiko wa leo umeanzisha safari ndefu ya kukuza lugha yetu ya Taifa toka
ngazi za chini hadi za kimataifa, hivyo Tanzania imefarijika kuwa mwenyeji wa
shughuli hii muhimu “alisema Mhe. Dkt. Mukangara.
Aliongeza kuwa kwa upande wa serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali
ya kukiendeleza Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya kufundishia kuanzi
shule ya Msingi hadi Elimu ya Juu.
Dkt. Mukangara ametoa wito kwa vijana kujifunza Kiswahili na kuitumia lugha
hiyo kuweza kujipatia ajira kwa kutangaza utumiaji wa bidhaa za lugha na
utamaduni ambazo zina thamani kubwa kiuchumi.
“Lugha ni sawa na kiwanda ikitumiwa vizuri italeta ajira kwa jamii husika na
kutumika kama lugha ya kufundisha wageni mbalimbali wanaokuja nchini na hata
nchi za nje kwa kuipa hadhi ya kuzungumzwa sehemu mbalimbali” alisema Mhe.
Dkt. Mukangara
Kwa Upande wa muandaaji wa tamasha hilo ambaye ni Rais wa Asasi za
Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Ali Akkiz amesema kuwa kupitia tamasha
hilo wameweza kutangaza vivutio mbalimbali vya kiutamaduni vya jijini Dar es
salaam na Zanzibar.
“Kwa kweli watoto wamefurahi kushiriki katika tamasha hili kwa kuweza
kutembelea sehemu zenye vivutio vya utamaduni pamoja na historia najua
wataondoka na taswira nzuri ya kutokuisahau nchi ya Tanzania” alisema Bw.
Akkiz
Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni ni la kumi 13 kufanyika ambalo
limeshirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 18 kutoka katika nchi 19
na nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tukio hili kwa mara ya kwanza.













Post a Comment