![]() |
| Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana |
UONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Mbeya,
umeombwa, kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya viongozi wa matawi katika
Jimbo la Mbeya Vijijini,ambao wamekuwa wanaoendesha siasa za ukabila.
Kauli hiyo imetolewa jana na wafuasi wa CCM, wakati
wakizungumza na Jamii moja blog, ambapo wamesema, viongozi hao wa matawi
wamekuwa wakiendesha kampeni za chini kwa chini, zenye mlengo wa kuwabeba
baadhi ya watu walionyesha nia ya kugombea nafasi za udiwani na ubunge, huku
wakitumia silaha ya ukabila.
Walisema,chama kinapaswa kuliona hilo na kuchukua hatua
za haraka kwani siasa za kupakana matope,ubaguzi dini, rangi na ukabila
zimepitwa na wakati.
Alisema, Jimbo la Mbeya vijijini limekuwa na sifa kubwa
ya ukabila lakini sifa hii imekuwa ikienezwa na viongozi wa kisiasa na si
wananchi ambao wao wamekuwa wakivitegemea vyama hivyo kuwapelekea viongozi
wenye sifa.
Aidha, alikitaka chama hicho kutoa nafasi kwa vijana
kuliongoza Jimbo hilo na kuachana na dhana za kizamani za kuwapa kipaumbele
wazee ambao tena ni wastaafu wa serikali ambao tayari wamelitumikia taifa hili.
“Chama kwa sasa kinatakiwa kuwalea wazee haona kuwatunza
kwani niamana kwa Taifa katika kutoa ushauri lakini si kushika
uongozi,”alisema.
Mwisho.







Post a Comment