![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi. |
WATU
nane wamepoteza maisha na wengine 6 kujeruhiwa baada ya gari lenye namba za
usajili T.599 AEG aina ya Fuso Mistubish kupinduka katika eneo la Maji mazuri,
Wilayani Mbeya.
Tukio
hilo limetokea leo jijini, majira ya saa mbili asubuhi katika Kijiji cha
Lwanjilo Wilayani Mbeya barabara Chunya/ Mbeya.
Kamanda
wa polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Kwa
upande wa majeruhi, Msangi alisema kuwa, watu sita wamejeruhiwa na kwamba
wanapatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Rufaa ya Mbeya.
Kamanda
Msangi ilisema, katika ajali hiyo watu saba walipoteza maisha papo hapo na
mwingine wa nane aliongezeka wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya
Rufaa ya Mbeya.
Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni kupinduka
kwa Lori la mizigo ambalo lilikuwa limepakia watu na mbao likiwa katika
mwendokasi eneo la maji mazuri Wilayani Mbeya kuacha njia na kupinduka.
Hata
hivyo, Msangi aliongeza kuwa polisi wanaendelea na msako wa dereva wa gari hilo
baada ya kufanikiwa kukimbia baada ya tukio hilo kutokea.







Post a Comment