Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania mwenye
beji ya FIFA, Israel Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Afrika (CL) kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi ya AS Kaloum ya
Guinea.
Katika mchezo huo
wa kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika kibendera John
Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri Sheha wote kutoka
Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin Shishana kutoka nchini
Afrika Kusini
Mchezo huo unatarajiwa
kufanyika kati ya tarehe 13,14,15 Machi mwaka huu nchini Zambia.
Post a Comment