Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameelezea masikitiko yake baada ya vifo vya watu wanane wengi wao raia wa Ufaransa.
Wanne
hao wanajumuisha pia wachezaji watatu wasifika nchini humo, walioaga
dunia baada ya ndege mbili za Helikopta kugongana angani nchini
Argentina.
Wakuu wametaja nyota hao kama bingwa wa nishani ya
dhahabu katika uogeleaji kwenye mashindano ya Olimpiki, Camille Muffat,
mwanandondi Alexis Vastine, na Florence Arthaud, gwiji katika mchezo wa
upigaji makasia.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi walipokua wakichukua picha za filamu.
Wanamichezo
nchini Ufaransa wameungana kutoa rambirambi zao kwa jamaa na marafiki
na haswa ulimwengu wa mechezo nchini humo kufuatia vifo vya nyota hao
katika ajali hiyo mbaya.
Marubani wote wawili raia wa Argentina walifariki pia katika ajali hiyo.
Vyombo vya usalama zinasema kuwa watu 10 waliangamia katika ajali hiyo.
Walikua wakirekodi picha za filamu maarufu ya "Dropped" inayoonyeshwa kwenye Televisheni ya Ufaransa, TF1.BBC SWAHILI
Post a Comment