Viongozi wa mashtaka nchini
Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa
ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150
alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa anaougua.
Maafisa
hao pia wamesema kuwa walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa
kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa
ndege hiyo.Hatahivyo hawakupata ujumbe wowote wa rubani huyo kutaka kujitoa uhai wake.
Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.
Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa alilazimika kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na shinikizo la akili.BBC SWAHILI
Post a Comment