Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumapili, Machi 2, 2015) kwenye uwanja wa CCM wa Vwawa wilayani Mboz |
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu Pinda |
SERIKALI imesema itajitahidi
kuhakikisha inalipa deni lote la mahindi yaliyonunuliwa kutoka kwa wakulima na
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ifikapo Machi 30, mwaka huu.
Akizungumza na maelfu ya
wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumapili, Machi 2, 2015)
kwenye uwanja wa CCM wa Vwawa wilayani Mbozi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema
Serikali imedhamiria kufuta deni lote.
Amesema kwa wialaya Mbozi serikali ilikuwa ikidaiwa sh. bilioni 21 lakini tayari seriali imetoa sh. bilioni 4.5 kwa hivyo kubakiwa na deni la sh. bilioni 16 ambalo litalipwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
“Tunachoweza kuahidi kama Serikali ni kwamba,
msimu huu hatutarudia kosa la mwaka jana ingawa mtihani mkubwa tulionao ni wa
kushughulika na hifadhi ya chakula kwa kujenga vihenge (SILOS) ili hata kama
kuna ziada n tusipate taabu ya kuhifadhi,” aliongeza.
Amesema alishakwenda Poland
kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete na wao wameshakuja kuona hali halisi
ilivyo. “Tumependekeza vihenge vijengwe kwenye kanda za Mbeya, Rukwa, Dodoma,
Dar es Salaam, Arusha au Kilimanjaro na Shinyanga ili iweze kuhudumia kanda ya
Ziwa,” alisema.
Wakati huo huo, Mbunge wa
Mbozi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi
amesema Serikali imekwishalipa zaidi ya sh. bilioni 81 na kwamba deni
lililosalia linafikia sh. bilioni 59.
“Hadi mwishoni mwa mwaka
jana, tulikuwa tumeshalipa sh. bilioni 51.5/- na mwaka huu tumepata sh. bilioni
15 kutoka CRDB na hivi majuzi kuna bilioni nyingine 15 zimetoka Hazina… Agizo
la Serikali ni kwamba mahindi yote yawe yamelipwa ifikapo Machi 30, naamini
tutakamilisha,” alifafanua.
Alielezea pia tatizo la maji
linaloukabili mji wa Mbozi na vitongoji vyake na kueleza kwamba Serikali
inashughulikia tatizo hilo katika programu mbalimbali.
Mapema, akiwa katika ghala la
nafaka la NFRA katika makao makuu ya wilaya ya Mbozi, Vwawa, Waziri Mkuu
alielezwa kwamba kanda ya Makambako ambayo inajumuisha vituo vya Makambako na
Vwawa imezidiwa uwezo na sasa wanalazimika kuhifadhi magunia ya mahindi nje kwa
vile maghala yamejaa.
Meneja wa Kanda hiyo wa NFRA,
Bw. Abdillah Nyangasa alisema kanda hiyo ina uwezo wa kuhifadhi tani za nafaka
34,000 ambapo kati ya hizo, tani 22,000 ni maghala ya Makambako na tani 12,000
ni maghala ya Vwawa, Mbozi.
Hata hivyo, Bw. Nyangasa
alisema kanda hiyo kwa sasa kina tani za mahindi 79,496.8 zikijumuisha tani
15,738.9 za msimu uliopita licha ya tani 63,757.8 ambazo zimenunuliwa katika
msimu huu.
“Ili kukabiliana na uhaba wa
maghala, kanda yetu hulazimika kufanya hifadhi ya nje (outside storage) kwa
kutumia maturubai (tarpaulins) ili mahindi yasiharibiwe na hali ya hewa kama
mvua au jua kali,” alisema Bw. Nyangasa.
Waziri Mkuu anamaliza ziara
yake ya siku saba mkoani Mbeya leo kwa kufanya majumuisho na kisha kurejea
jijini Dar es Salaam.
Mwisho
Post a Comment