Katika hali isiyokuwa ya
kawaida Mbunge wa Jimbo la Songwe Mheshimiwa PhilIp Mulogo ameduwaza wananchi na wapiga kura wake
wa jimbo lake la songwe kwa kitendo chake cha kupiga magoti mbele ya waziri Mkuu
Mizengo Pinda kwa lengo la kumshinikiza waziri huyo kutoa tamko juu ya lini
barabara ya Mbalizi chunya itakamilika kwa kuwekewa lami.
Hatua hiyo ilikuja katika
Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbuyuni Kata ya Gua jimbo la Songwe ambapo mbunge alitakiwa kutoa neno la shukrani na kusalimia wananchi mara
baada ya waziri mkuu kudhuru katika halmashauri hiyo ya chunya ikiwa ni sehemu
yake ya ziara iliyolenga kutembelea shughuli mbalimbali za kimaendeleo
zinazotekelezwa na serikali pamoja na washirika wa maendeleo katika mkoa wa
mbeya.
Mbunge huyo mara baada ya kutoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu ghafla alipiga magoti na kutoa maneno ya
huruma kwa kumtaka Waziri Mkuu Pinda kutoa tamko kwa wananchi juu ya lini barabara ya Mbalizi Mkwajuni itakamilika kwa wakati na kuondoa kero kwa
wananchi wa jimbo lake hali ambayo iliibua mshangao mkubwa kwa wananchi na wapiga kura wake.
Akiongea mara baada ya
kupiga magoti huku akimtazama Mheshimiwa Pinda alisema kuwa amekuwa na mtihani
mkubwa kwa wananchi wake kuhusiana na
kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo imekuwa ikizungumzwa mara kwa mara na serikali kuwa ipo katika mikakakati ya kujengwa.
Amesema kero kubwa waliyo
nayo kwa sasa wananchi wa jimbo hilo ni ubovu wa barabara hiyo kwani ndio
kiungo kikubwa cha kusukuma maendeleo katika jimbo lake la Songwe .
Pamoja na kuibua hoja hiyo
Pia mheshimiwa Mulugo alimuomba
Mheshimiwa waziri Mkuu kulipa nguvu za kutosha suala la uanzishwaji wa Wilaya
katika jimbo hilo ambalo makao makuu yake yamependekezwa kuwa Mkwajuni
Akizungumzia hoja hizo za Mbunge kwa kuanza na suala la
barabara Mheshimiwa Pinda alisema tayari hatua za awali zimekwisha fanyika kwa kwa kuufanyika
upembuzi yakinifu hivyo amewataka wananchi wa jimbo la songwe pamoja na mbunge
huyo kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na mchakato huo.
Amesema pamoja na juhudi hizo pia atajalibu kuzunguzma na Waziri Magufuli ili kufahamu kwa kina juu ya kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo ya Chunya Mbalizi yenye kilomita 60 .
Kuhusiana na
ombila kuanzishwa kwa Wilaya katika jimbo hilo Waziri Mkuu Pinda amesema tayari
wamekwisha pokea ombi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) cha Mkoa wa
Mbeya yanayopendekeza mkoa huo ugawanywe na kupata mikoa miwili ya Mbeya na
Songwe.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda amesema Serikali imeridhia maombi hayo kutokana na ukubwa wa mkoa
huo ambao una kilometa za mraba 63,000 ambapo nusu yake ni Wilaya ya Cunya.
Amesema
kamati hiyo imeshauri mkoa huo ugawanywe katika wilaya nne nne ambapo mkoa mpya
wa Songwe utakuwa na wilaya za Ileje, Momba, Mbozi na Chunya.
Alisema
katika kikao hicho ilikubaliwa kwamba makao makuu ya wilaya mpya ya Songwe
yatakuwa Mkwajuni .
.
“Nimekubali maombi haya kwa sababu yatapunguza gharama za uendeshaji, na kama
itashindikana kupata wilaya mpya basi itabidi tuwape Halmashauri ya Songwe,”
alisema.
Mkoa
wa Mbeya una wilaya nane ambazo zimegawanyika katika tarafa 27, kata 262,
vijiji 842 na mitaa 252. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012 ni 2,707,410.
Mwisho
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment