Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akimjulia hali mmoja wa askari waliopata ajali wakati msafara wake ukielekea Kata ya Galula wilayani Chunya mpakani mwa Chunya na Mbeya. |
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akitoka katika hospital ya Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwatembelea majeruhi wa ajali hiyo. |
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amewatembelea askari wa Jeshi la Polisi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa
Mbeya kutokana na ajali waliyoipata jana wakati msafara wake ukielekea Kata ya
Galula wilayani Chunya.
Waziri Mkuu aliwatembelea
majeruhi hao na kuwapa pole leo asubuhi (Jumapili, Machi Mosi, 2015) kabla ya
kuelekea wilayani Mbozi kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Mbeya. Alifuatana na
mkewe Mama Tunu Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro na Mganga Mkuu
wa Mkoa huo, Dk. Seif Mhina.
Akizungumzia hali ya majeruhi
hao, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ismail Macha alisema jana walipokea
majeruhi tisa lakini watatu walifanyiwa uchunguzi wa afya zao na kuruhusiwa na
wengine sita ilibidi wawalaze na kuwafanyia uchunguzi zaidi kutokana na hali
zao zilivyokuwa.
Aliwataja waliolazwa kuwa ni
Deogratius Nandi (31), Paulin Masolwa (27), Omary Hussein (24), Hamisi Haji
(29) ambao wote ni wanaume. Majeruhi wa kike ni Cecilia Mussa Kabona (28) na
Mwazanije Hassan (23) ambaye amevunjika mkono wa kulia. Waliopata matibabu na
kuruhusiwa ni Mashaka Shabani (42), Khalifa Rashid (26) na Joel Cheja (21).
Dk. Macha alisema wanatarajia
kuwaruhusu leo mchana ama kesho asubuhi kwani hali zao zinaendelea vizuri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni vumbi na kokoto barabarani
ambazo zilifanya gari hilo la FFU lisesereke na kupinduka. Hata hivyo, alisema
mwendo mdogo wa gari hilo ulisaidia kuokoa maisha ya askari hao.
Waziri Mkuu leo amemaliza ziara yake yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Mbozi ambapo mbali ya
kuzungumza na wananchi, amezindua maabara Vwawa sekondari, nakugua ghala la
nafaka la NFRA na kupokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji wa miche ya
kahawa kwenye kituo cha TACRI – Mbimba.
Mwisho.
Jamiimojablog
Post a Comment