MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBEWE WILAYANI MBOZI AMEUAWA
KWA KUKATWA NA KITU CHENYE KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI
WA KIJIJI CHA MBEWE WILAYANI MBOZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FERUZI JAGRAS (36) ALIKUTWA AMEUAWA KWA
KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI MARA TANO NA SHINGONI MARA
MOJA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE MTO MUYOVIZI ULIOPO WILAYANI MBOZI.
MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA KWENYE MTO HUO MNAMO TAREHE
03.03.2015 MAJIRA YA SAA 15:00
ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOMORA, KATA YA MALANGALI, TARAFA YA IYULA,
WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA INADAIWA
KUWA, MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE TANGU TAREHE 26.02.2015 KWENDA MATEMBEZINI KUSIKOJULIKANA. WATUHUMIWA
WAWILI WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. PADRI MWIWA (48) MKAZI WA MBEWE NA 2. PETER MWAMENGO (51) MKAZI WA LUKULULU.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AITWAYE MAISHA
CHRISTOPHER (46) AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA
MBILI [02].
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2015
MAJIRA YA SAA 14:01 MCHANA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NILE MWALYEMBELE (58) NA 2. OSWARD MWANGOMOLE (40) WAKIWA NA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05].
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2015
MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
AIDHA
KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AITWAYE GODLUCK JOSEPH (18) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 183 ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 915.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2015
MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO
KATIKA ENEO LA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA [BHANGI] NA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU
KIKUNDI CHA WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA DAWA ZA
KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment