Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Na Baraka Kizuguto,Dar es salaam
Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kucheza na timu ya Taifa ya Misri siku ya ijumaa majira ya saa 10 kamili jioni, mchezo utakofanyika katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo, ambapo kwa takribani wiki mbili kipo kambini Bamba Beach wakijifua kwa mchezo huo.

Tanzania ilifuzu hatua ya pili baada ya kuiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12 -9, na endapo itafanikiwa kuwaota Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli mwezi April  mwaka huu.

Waamuzi wa mchezo huo ni Eid Haitham Eid Hassan (Sudan), mwamuzi msaidzi wa kwanza  Abaker Mohamed Bilal (Sudan), mwamuzi msaidizi wa pili Abdalla Hassain Hassaballa, mtunza muda (time-keeper) Boubaker Bessem (Tunisia) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Khiba Herbert Mohoanyane kutoka Lesotho.

Nayo timu ya Taifa ya Misri inatarajiwa kuwasili Dar es salaam kesho (jumatano) mchana, ambapo itafikia katika hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Masaki, huku waamuzi wa mchezo huo wakitarajiwa pia kuwasili kesho na kufikia katika hotel ya Protea Oysterbay.

Aidha siku ya alhamis makocha wa timu zote wataongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume kuanzia majira ya saa 5 kamili asubuhi.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Misri kati ya Machi 20,21 na 22 mwaka huu.

Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), inaitakia kila la kheri na ushindi timu ya Taifa ya soka la ufukweni (Beach Soccer) katika huo dhidi ya Misri.
Wakati huo huo michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyokuwa iichezwe kesho (jumatano)  kati ya JKT Ruvu dhidi ya Young Africans katika uwanja wa Taifa, na Mgambo Shooting dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga imeahirishwa  na sasa mechi hizo zitapangiwa tarehe nyingine.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top