Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kuelekea mpambano  wa watani wa jadi katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini, mchezo kati ya Simba na Yanga ambao utafanyika hapo kesho kwenye uwanja wa taifa jiji Dar, Staa wa Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’ ambae ni mshabiki “kindakindaki” wa timu ya Simba amemtaka Staa mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’  ambae ni shabiki wa Yanga, aweke dau shilingi milioni moja kama alivyofanya mchezo uliopita na yeye JB ataweka milioni mbili, kama Yanga ikishinda Ray atachukua mzigo na kama Simba ikishinda JB atachukua mzigo huo.
“Weka milion, mimi naweka mbili sheria zinasema mwenye uhakika wa ushindi ana point chache.si haki tukiweka sawa..si unakumbuka mara ya mwisho tulipokutana.jaribu tena urudishe hela yako...”-JB aliandika na kumtag Ray mara baada ya kuweka picha hiyo wakiwa pamoja.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top