Na Mwandishi wetu,Mbozi
Kituo cha utafiti wa zao la kahawa
cha TacrI Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya na Katavi kimeendelea na juhudi
mbalimbali zaa kuhakikisha kinaongeza zaidi ubora wa kahawa
kutoka daraja 9,13 hadi 5 na 9.
Akizungumza
Meneja kituo hicho cha utafiti wa zao la
kahawa kilichopo Mbimba Mbozi Ndugu Isack Mushi amesema katika kufikia lengo
hilo kituo hicho kimenza na jitihada za kuongeza uzalishaji kwa mti wa kahawa
kutoka gramu 250 hadi kufikia walau gramu 1000 ambayo ni sawa na kilo moja.
Amesema hatua nyingine ni
kuongeza uzalishaji wa miche bora ya kahawa ili kukidhi mahiyaji ya wakulima
sanjali na kukagua rutuba ya udongo wa
maeneo ya kahawa na kutoa mapendekezo muafaka ya urutubishaji.
Aidha Meneja huyo amesema
kuwa zipo changamoto mablimbali ambazo kituo hicho kinakabiliana nazo ambazo ni
pamoja na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti ya utafiti kutoka serikalini.
Amesema changamoto nyingine
ni uwekezaji hafifu wa halmashauri za wilaya katika kuendeleza kilimo cha
kahawa.
Kutokana na changamoto hizo
Meneja huyo ameitaka serikali kuhakikisha inaongeza bajeti yake katika
kugharamia shughuli za utatifi wa zao hilo.
Awali katika ziara yake hivi
karibuni Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwataka maafisa kilimo katika halmashauri hiyo
kutoa elimu kwa wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanaendeleza kilimo hicho kwa
kufuata taratibu bora za kilimo hicho.
Zao la kahawa likiwa shambani |
Government should put much efforts to support this sector in order to push up sector further for coffee
ReplyDelete