|
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika
hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania,
Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo
tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na
Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. | |
|
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika
hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania,
Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo
tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na
Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. |
|
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa shukrani kwa uongozi wa NSSF
mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi anuai ya NSSF
jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi
ya Bunge. |
|
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar
es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa
ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. | |
|
Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Kigamboni. |
|
Baadhi
ya viongozi wa NSSF wakimuongoza Spika wa Bunge la Tanzania, Anne
Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge katika ziara yao
ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam. |
|
Naibu
Katibu Mkuu, Joseph Nyamuanga (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya
pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa
daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha
Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. |
|
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na
NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa
Kigamboni. |
|
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa
Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la
Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge
walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam
ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na
Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. |
|
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na
NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa
Kigamboni. Mwenye kanzu ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau. |
|
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (aliyenyoosha mkono) akielezea
maendeleo ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda
pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa
daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha
Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. |
|
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na
NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa
Kigamboni. |
|
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (wa pili kushoto mbele) akitoa
ufafanuzi juu ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda
pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa
daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha
Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.CREDIT MICHUZI |
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amelipongeza Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa miradi mikubwa mbalimbali linayoendelea
kuwekeza nchini ambayo imekuwa chachu ya maendeleo na kukuza hadhi ya
nchini.
Spika
Makinda ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akitembelea baadhi ya miradi
mikubwa ya NSSF iliyopo jijini Dar es Salaam, ukiwemo mradi wa ujenzi wa
daraja la kubwa la kisasa linalojengwa kuunganisha Jiji la Dar es
Salaam na Mji wa Kigamboni pamoja na mradi mkubwa wa ujenzi wa Mji wa
Kisasa unaojulikana kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa kwa ubia
pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa zenye hadhi mbalimbali kulingana na
mahitaji ya watu.
Akizungumza
wakati akitembelea miradi hiyo, Makinda alisema miradi hiyo mbali na
kuleta maendeleo nchini inakuza hadhi ya nchi pamoja na kuirahisishia
serikali katika utoaji huduma kwa wananchi wake.
Aliiomba Serikali kupitia Wizara mbalimbali na jamii nzima kuendelea
kutoa ushirikiano dhidi ya miradi hiyo kwani inachangia maendeleo
kuanzia ngazi ya jamii pamoja na taifa kwa ujumla.
Aliwataka
wananchi kutumia fursa iliyopo ya kununua na kukopa nyumba zinazojengwa
na shirika hilo kwani mbali na kujengwa kwa hadhi anuai na kisasa
zimepangiliwa jambo ambalo linarahisisha utoaji wa huduma za jamii dhidi
yao.
Alisema kwa maendeleo ya sasa ni nchi ya Tanzania pekee ambapo raia wake
hujenga nyumba wenyewe, kwani mataifa mengi yaliyoendelea nyumba
hujengwa na mashirika na kuuzwa kwa raia jambo ambalo huchangia kwa
kiasi kikubwa uwepo wa miji iliyopangiliwa tofauti na ilivyo Tanzania.
"...Duniani kote watu wanaojenga nyumba wenyewe hadi sasa ni Tanzania
tu, na hii ndio chanzo kikubwa cha nchi yetu kuendelea na kuwa na miji
ambayo haijapangiliwa (ujenzi holela).
Lazima
tubadilike unajua ukiwa na mji uliopangiliwa ni rahisi hata kuwahudumia
wananchi wako...," alisema Makinda.
Aidha alishauri uwepo wa utaratibu mzuri wa kukopesha nyumba za kisasa
zinazojengwa na NSSF ili wahitaji wapewe na kulipa kwa awamu huku
wakimilikishwa nyumba hizo jambo ambalo litaondoa adha ya upatikanaji wa
makazi bora kwa wananchi.
Katika ziara hiyo Spika Makinda aliambatana na Waziri wa Fedha Saada
Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),
Jenista Mhagama , Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka pamoja na
Kamati ya Uongozi ya Bunge la Tanzania ambao kwa pamoja walilipongeza
Shirika la NSSF na kushauri kuendelea kuwekeza pia katika mikoa mingine
inayochipukia kimaendeleo kwa sasa ili kusambaza huduma maendeleo
mengine.
Awali
akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni,
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa alisema licha ya changamoto
zilizojitokeza mradi huo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 75 ya ujenzi
wake.
Kwa upande wake, Mhandisi Juhus Nyamuhokya wa kampuni ya Ujenzi ya
Hifadhi wabia wa NSSF katika ujenzi wa Kijiji cha kisasa cha 'Dege ECO
Village' kinachojumuisha ujenzi wa nyumba 7,460 za kisasa zenye hadhi
tofauti kulingana na mahitaji alisema ujenzi wake utajumuisha miaka
minne ukijengwa kwa awamu tatu.
Mhandisi
Nyamuhokya alisema awamu ya kwanza ya mradi huo inakamilika Desemba
2015, awamu ya pili itakamilika Desemba 2016 huku awamu nyingine
ikitarajiwa kukamilika Desemba 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau alimshukuru Spika wa Bunge la
Tanzania Anne Makinda pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge
kwa kutembelea miradi hiyo ambayo ina lengo lakuchochea maendeleo ya
taifa na wananchi kiujumla.
Post a Comment