|
Baadhi ya majirani wa mtaa wa Hayanga RRM jijini Mbeya wakiwa nje ya nyumba ambapo tukio hilo limetokea . |
|
Waombolezaji |
Watu wawili wafanyakazi shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Mbeya Ndugu
Uswege Mwankuge (58) na Jusio Uswege (48) ambao ni mtu na mke wake wamekutwa
wamekufa ndani ya nyumba yao mtaa hayanga RRM jijini mbeya .
Tukio hilo la kusikitisha
limetokea leo jijini hapa ambapo inadaiwa kuwa wawili hao wamekutwa wamekufa ndani
ya nyumba yao usiku wa kuamkia leo Marchi 3 mwaka huu
Akizungumiza tukio hilo
Balozi wa mtaa huo Jofrey Katuli amesema yeye alipigiwa simu majira ya saa 4
asubuhi kuwa Ndugu Uswege Mwankuge
pamoja na mke wake ndugu Jusio Uswege wamekufa wakiwa ndani ya nyumba yao .
Amesema watoto wa marehemu ndio waliogundua
kuwepo kuwepo kwa tukio hilo kutokana kuwepo kwa
ukimywa wa muda mrefu ndani ya chumba cha wazazi wao ambapo walilazimika kuingia
chumbani na kumkuta baba na mama yao tayari wakiwa wamekufa .
Amesema baada ya kugonga kwa
muda mrefu bila kufunguliwa walilazimika kubomoa mlango ambapo walikuta baba
yao akiwa amening'inia juu huku tayari akiwa amekufa kwa kujinyonga ambapo
mama naye alikuwa amelala kitandani huku
akiwa amekwisha fariki ambapo mwili wake ukiwa na majeraha shemu za usoni.
Amesema baada ya kupata maelezo
hayo walipiga simu kituo cha Polisi ambapo walifika na kuchukua miili ya watu
hao na kuipelekea hospital ya rufaa Mbeya kwa ajiri ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa balozi huyo amedai kuwa
inawezekana kuwa mwanaume huyo ambaye sasa ni marehemu alimuua mke wake kwa kumpiga na kitu kizito
kichwani hadi kufa kuku yeye akijaribu kujiua kwa kutumia sumu ambayo
ilishindikana na kutumia mbinu ya
kujinyonga ambayo aklifanikiwa nayo.
Mmoja wa Majirani wa marehemu hao
Ndugu Alex Kyabyara amesema hawakuwahi kusikia ugomvi wa aina
yeyote baina ya wawili hao hivyo tukio
hilo limewastaajabisha huku wakishindwa kujua nini chanzo cha mauji hayo.
Akithibisha kutokea kwa tukio
hilo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Ahmed Msangi amesema tukio
hilo limetokea majira ya saa Nne asubuhi ambapo amedai kuwa watu hao walikuwa
na ungomvi usiku wa manane hali ambayo imepelekea mauiji hayo.
Aidha kamanda msangi amekili kuwa
wawili hao ambao ni mke na mume bado walikuwa ni watumishi wa shirika la umeme
tanesco mkoa wa mbeya hadi umauti huo unawakuta.
Amesema bado uchunguzi zaidi
unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha mauiji hayo ambapo miili ya
marehemu hao imehifadhiwa katika hospital ya rufaa jijini Mbeya.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment