Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.


Watu watatu  wamefariki Dunia mkoani mbeya mara baada ya kuangukiwa na kifusi wakiwa katika shughuli za uchimbaji madini.

Tukio hilo limetokea March 11,mwaka huu saa 1:15 jioni huko katika kitongoji cha Mawowo, kijiji cha patamela, wilayani chunya, huku chanzo cha tukio hilo ni baada ya kuta za shimo kuloa maji na kukosa uimara na kisha kuporomoka.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Ahmed Msangi amewataja waliofariki dunia kuwa ni Victor Sanga (26) mkazi wa mbeya,mwingine amefahamika kwa jina moja la sheta umri kati ya miaka 30-35 na watatu hajafahamika jina wala makazi, jinsi ya kiume, umri kati ya miaka 30.

Amesema  wote wachimbaji wadogowadogo wa madini ya dhahabu walikutwa wamekufa kwenye shimo lenye urefu wa futi 50 walimokuwa wakichimba dhahabu baada ya kuangukiwa na kifusi.

Kamanda Msangi amesema miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya mwambani chunya huku upelelezi zaidi wa tukio hili unaendelea.
Mwisho
JAMIIMOJABLOG

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top