Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo |
WALIMU wa shule ya Sekondari
yaTotowe na shule ya Msingi Mpona zilizopo katika Kata ya Malangali Wilayani
Chunya Mkoa wa Mbeya, wamegoma kuendelea kufundisha baada ya kuchoshwa na
vitendo vya vitisho wanavyotolewa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.
Wamesema,vitisho hivyo
vimekuwa vikitolewa na baadhi ya watu ambao, wameunda kikundi kinachotambulika
kwa jina la “Watu Pori” ambacho kimekuwa kikutumia kauli za maneno kutoa
vitisho hivyo vya kuwaua walimu hao ikiwa na kwa njia ya maandishi.
Akizungumza na Blog hii Mwalimu Iddy Puga wa shule ya msingi ya Totowe, alisema kundi hilo limekuwa
likiwatishia kuwaua jambo ambalo linawafanya washindwe kufanya kazi zao vizuri,
hivyo wameamua kuachana na kazi hiyo ya kuwafundisha watoto ili kuokoa uhai wao.
Alisema, tatizo kubwa
linalosababisha kuwepo kwa vitisho hivyo ni baada ya walimu wa shule hizo
kuweka misimamo ikiwa na kusimamia sheria ya serikali inayowataka watoto wote
waliofikisha umri wa kusoma kuingia darasani hususani kwa jamii ya wafugaji
ambayo iko nyuma kielimu.
Alisema, kutokana na vitisho
hivyo waalimu wa shule hizo wameingiwa na hofu jambo ambalo limewafanya
kushindwa kwenda shule kuendelea na utoaji wa huduma ya elimu kwa wanafunzi.
Akiongelea tatizo hilo kwa
njia ya simu Mkurugenzi wa halamshauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumburi, alisema
ofisi yake imepokea taarifa hiyo na kwamba inaendelea kulishughulikia, hata hivyo
ameitaka jamii kutambua kuwa wanawajibu mkubwa wa kuwalinda watumishi wa
halamashuri wanaopelekwa katika vijiji vyao ili kurahisisha huduma za
kimaendeleo.
Hata hivyo, alisema kamati
ya ulinzi na usalama wilaya ya Chunya inatarajia kufanya mkutano na wakazi wa
kata hiyo ya Malangali ili kutafuta suluhisho la kudumu dhidi ya vitisho hivyo
vya watumishi wa Serikali.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment