Na Saimeni Mgalula-Mbeya
WENYEVITI wa serikali za mitaa kupitia tiketi ya chama chama
cha democrasia na maendeleo(chadema) wilayani Ileje mkoani Mbeya watakiwa kuwasomea
wananchi mapato na matumizi ili wajue
mwenendo wa kodi zao.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha democrasia na
maendeleo (chadema ) mkoa wa Mbeya Joseph Mwachembe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana
katika kijiji cha Malangali kata ya malangali wilayani humo.
Alisema fedha zinazotumika na viongozi katika shughuli za maendeleo
mbalimbali ni kodi ya wananchi wenyewe hivyo hawana budi ya kufahamu mwenendo
mzima wa fedha zao.
“Kila kiongozi aliyeshinda katika serikali za mitaa kwa
tiketi ya chama cha democrasia na maendeleo katika uchaguzi wa serikali za
mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana anapaswa kuwa mwajibikaji na siomzigo kwa waliompigia kura” alisema Mwachembe.
Alisema tumepata malalamiko mengi kwa wananchi kuwa kuna
baadhi ya viongozi hawawasomei wananchi mapato na matumizi huku wakitumia fedha za wananchi kwa masirahi
binafsi, kinyume cha irani ya chama cha democrasia na maendeleo watawajibishwa.
“Kama kuna kiongozi yeyote ambaealikuwa anawania uongozi
kupitia tiketi ya chadema kuwa amepata ajira na niwakati wake katika kunufaika
yeye binafsi kwa a kutafuna fedha za watanzania , kama wapo wajiuzulu mapema kabla ajawajibishwa na chama
na aludishe kadi ya chama “ alisema.
Sanjali na hayo Mwachembe aliwataka wanaileje waliotia nia kuwania ubunge katika Jimbo la
wilaya hiyo kwa tiketi ya chama cha democrsia na maendeo, kutumia rushwa katika kujinadi waache mala moja maana rushwa
ni adui wa haki.
Alisema kiongozi yeyote anaetoa rushwa hana nia nzuri na
wananchi, malengo yake ni kwenda kuchuma
na sio kuwawajibikiwa waliompigia kura kwa kutuia fedha za maendeleo ya wananchi katika shughuli zake binafsi.
“Kura hazinunuliwi kwa fedha, haki ainunuliwi, kupiga kura
nia haki ya kila mtanzanaia hivyo wana Ileje msidanganyike na watia niawote wanaotoa rushwa na hili ni kwa vyama vyote
hapa nchini” alisema Mwachembe.
“Wananchi mkiletewa
fedha na mgombea yeyote anaetaka Udiwani, Ubunge na Uraisi mkataeni , mwambie
kupiga kura ni haki yenu hivyo hatudanganyiki kwa pesa” alisema.
Mwisho.
Post a Comment